“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari
ya kila siku
Jumanne,
Oktoba 27, 2020,
Juma
la 30 la Mwaka wa Kanisa
Ef
5: 21-33;
Zab
128: 1-5;
Lk
13: 18-21
UFALME
WA MUNGU-UPO NA BADO UTAKAMILIKA
Karibuni
ndugu zangu kwa tafakari ya neno la Mungu katika adhimisho la Misa Takatifu asubuhi
ya leo. Leo basi tafakari yetu inaanza kwa kuiangalia zaburi yetu ya wimbo wa
katikati ambapo tunamkuta mzaburi akielezea juu ya faida atakayoipata yeyote
yule amchaye Bwana. Familia yake itakuwa na utulivu na yeye atafurahia kuishi
ndani yake.
Hapa
twajifunza kwamba kumcha Bwana ndio chanzo cha baraka ndani ya familia na
kinachokusaidia ufurahie kuishi ndani ya familia. Baadhi yetu kwa siku zetu
hizi hatufurahii maisha ndani ya familia zetu, tunapata raha zaidi tukiwa nje
ya familia kuliko tukiwa ndani. Familia inakuwa kama gereza. Tuanze kwa kumcha
Bwana na maisha ndani ya familia yatavutia zaidi.
Tumemtupa
Bwana, tumeacha kusali pamoja na hiki ndicho chanzo cha chuki ndani ya familia.
Hata fundisho linaloelezewa na Paulo katika somo la kwanza linaeleweka kwa
familia inayosali. Familia inayojali sala ndiyo inayoweza kuishi maisha ya
utulivu na kutumikiana, ya mke kumtambua mume wake kama kichwa cha familia na
ya mume kumwona mke wake kama sehemu ya mwili wake. Bila sala ndani ya familia
hili fundisho halieleweki. Tukizidishe sala hili litakuwa fundisho rahisi. Sala
huifanya familia ipendeze, ivutie, iwe kama ua. Tuzidishe sala ndani ya familia
zetu.
Katika
injili Yesu anatumia mfano wa punje ya haradali na chachu kuelezea namna ufalme
wa mbinguni unavyoanza kwa mambo madogo madogo na kuweza kupanuka na kuwa
makubwa zaidi.
Familia
ni kiungo muhimu kwa maisha ya mkristo yeyote. Tukizijenga familia zetu kwa
sala, kila mmoja wetu akifanya hivyo ama kweli tutamjengea Mwenyezi Mungu
ufalme mkuu kabisa. Familia zetu ndio kitalu cha ufalme wa mbinguni. Tujitahidi
imani, utulivu, furaha, amani vifunike familia zetu. Huu utakuwa mchango mkubwa
sana katika uinjilishaji.
Pia
yote aliotupa Mungu iwe ni kipaji au chochote hata kama tunaona ni kidogo
tukitumie kwa upendo utashangaa kitakuwa, na sisi wenyewe tutasitawi na wengine
watapata kivuli chini ya kile tulichokikuza kwa upendo alichotupatia Mungu.
------------------------
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment