MASOMO YA MISA, OKTOBA 27, 2020
JUMANNE,
JUMA LA 30 LA MWAKA
SOMO
1
Efe.
5:21 – 33
Hali
mnanyenyekeana katika kicho cha Kristo. Enyi wake, watiini waume zenu kama
kumtii Bwana wetu. Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni
kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili. Lakini kama vile Kanisa limtiivyo
Kristo, vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo.
Enyi
waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa
ajili yake; ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno; apate
kujiletea Kanisa atukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wal alolote kama hayo;
bali liwe takatifu lisilo na mawaa. Vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda
wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda wenyewe. Maana
hakuna mtu anayeuchukia mwili wake popote; bali huulisha na kuutunza, kama
Kristo naye navyolitendea Kanisa. Kwa kuwa tu viungo vya mwili wake. Kwa sababu
hiyo mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe na hao wawili
watakuwa mwili mmoja.
Siri
hiyo ni kubwa; ila mimi nanena habari ya Kristo na Kanisa. Lakini kila mtu
ampende mke wake kama nafsi yake mwenyewe; wala mke asikose kumstahi mumewe.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
128:1 – 5 (K)
(K)
Heri kila mtu amchaye Bwana.
Heri
kila mtu amchaye Bwana,
Aendaye
katika njia yake.
Taabu
ya mikono yako hakika utaila;
Utakuwa
heri, na kwako kwema. (K)
Mkeo
atakuwa kama mzabibu uzaao,
Vyumbani
mwa nyumba yako.
Wanao
kama miche ya mizeituni
Wakiizunguka
meza yako. (K)
Tazama,
atabarikiwa hivyo, yule amchaye Bwana.
Bwana
akubariki toka Sayuni;
Uone
uheri wa Yerusalemu siku zote za maisha yako. (K)
SHANGILIO
1Pet.
1:25
Aleluya,
aleluya,
Neno
la Bwana hudumu hata milele, na neno hilo ni neno lile jema lililohubiriwa
kwenu.
Aleluya.
INJILI
Lk.
13:18-21
Yesu
alisema, Ufalme wa Mungu umefanana na nini? Nami niufananishe na nini?
Umefanana na punji ya haradali aliyotwaa mtu akaitupa katika shamba lake;
ikamea, ikawa mti; ndege wa angani wakakaa katika matawi yake.
Akasema
mara ya pili, Niufananishe na nini ufalme wa Mungu? Umefanana na chachu
aliyotwaa mwanamke akaisitiri ndani ya pichi tatu za unga, hata ukachacha wote
pia.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.
-------------------------
No comments:
Post a Comment