MASOMO
YA MISA, OKTOBA 29, 2020
ALHAMISI,
JUMA LA 30 LA MWAKA WA KANISA
SOMO
1
Efe.
6:10 – 20
Mzidi
kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. Vaeni silaha zote za
Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. Kwa maana kushindana kwetu sisi
si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya nyama; bali ni
juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo
wabaya katika ulimwengu war oho. Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu,
mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.
Basi
simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani, na
kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya mani; zaidi ya yote mkitwaa ngao
ya Imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule
mwovu.
Tena
ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu; kwa sala
zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na
kudumu katika kuwaombea watakatifu wote; pia na kwa ajili yangu mimi, nipewe
usemi kwa kufumbua kinywa changu, ili niihubiri kwa ujasiri ile siri ya Injili;
ambayo kwa ajili yake mimi ni mjumbe katika minyororo; hata nipate ujasiri
katika hiyo kunena jinsi inipasavyo kunena.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
144:1 – 2, 9 – 10 (K) 1
(K)
Ahimidiwe Bwana, mwamba wangu.
Ahimidiwe
Bwana, mwamba wangu,
Anifundishaye
mikono yangu vita,
Vidole
vyangu kupigana. (K)
Mhisani
wangu na boma langu,
Ngome
yangu na mwokozi wangu,
Ngao
yangu niliyemkimbilia,
Huwatiisha
watu wangu chini yangu. (K)
Ee
Mungu, nitakuimbia wimbo mpya,
Kwa
kinanda chenye nyuzi kumi nitakuimbia.
Awapaye
wafalme wokovu,
Amwokoa
Daudi, mtumishi wake, na upanga wa uovu. (K)
SHANGILIO
Zab.
119:18
Aleluya,
aleluya,
Unifumbue
macho yangu niyatazame maajabu yatokayo katika sheria yako.
Aleluya.
INJILI
Lk.
13:31-35
Saa
ile ile, Mafarisayo kadha wa kadha walimwendea Yesu, wakamwambia, Toka hapa,
uende mahali pengine, kwa sababu Herode anataka kukuua. Akawaambia, Nendeni,
mkamwambie yule mbweha, Tazama, leo na kesho natoa pepo na kuponya wagonjwa,
siku ya tatu nakamilika. Pamoja na hayo imenipasa kushika njia yangu leo na
kesho na kesho kutwa; kwa kuwa haimkini nabii aangamie nje ya Yerusalemu.
Ee
Yerusalemu, Yerusalemu, uwauaye manabii na kuwapiga kwa mawe waliotumwa kwako,
mara ngapi nimetaka kuwakusanya watoto wako kama vile kuku avikusanyavyo
vifaranga vyake chini ya
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment