Everyday Saint / Maisha ya Watakatifu

KUSALI BILA KUCHOKA!

 

“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”

Alhamisi, Oktoba 29, 2020,

Juma la 30 la Mwaka wa Kanisa

 

Efe 6:10-20;

Zab 143:1-2, 9-10;

Lk 13:31-35

 

 

KUSALI BILA KUCHOKA!

 

Lengo la Barua kwa Waefeso ina lenga kujenga jumuiya ya Wakristo iliyo na upendo na umoja. Leo tuna maelekezo ya mwisho “salini nyakati zote daima katika Roho”. Mara nyingi sala zetu zinaishia katika kusema kwa fomula flani au kutafakari vifungu flani vya maandiko au tukiomba mahitaji yetu kutoka kwa Mungu na kwa kupitia kwa watakatifu.

 

Sala ni upendo wa kila mara kwa Mungu au “muonekano wetu unajiweka mbele ya Mungu” (Mt. Yohane Paulo II). Kusali nikuwa na umoja wa upendo wa ndani na Mungu, kushiriki kwenye upendo usio na mwisho wa Mungu. Ni kujiunga kwa mtu na Mungu katika muungano wa ndani. Hii inawezekana katika ukimya wa moyo. Uhusiano huu unaweza kujengwa tuu, kwa njia ya maisha ya fadhila. Hili ndilo tunalosikia katika somo la leo. Tunaalikwa tuwe makini dhidi ya ujanja wa yule muovu, tuzitambue mbinu zake katika jitihada zetu za kutaka kuwa na Mungu, kuwa mwaminifu, mwenye haki na mwenye Amani ya Injili. Maisha yetu ya fadhila yatakuwa ni maisha ya kusali daima katika Roho.

 

Sala. Ee Bwana, ninaomba unipe fadhila zote zinazo hitajika katika hali yangu ya maisha ili niweze kukuwa katika maisha yangu ya sala. Amina

 

------------------------

Copyright ©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.

No comments:

Post a Comment