MASOMO
YA MISA, OKTOBA 21, 2020
JUMATANO,
JUMA LA 29 LA MWAKA
SOMO
1
Efe.
3:2 – 12
Mmesikia
habari ya uwakili wa neema ya Mungu niliyopewa kwa ajili yenu; ya kwamba kw
akufunuliwa nalijulishwa siri hiyo, kama nilivyotangulia kuandika kwa maneno
machache. Kwa hayo, myasomapo, mtaweza kuutambua ufahamu wangu katika siri yake
Kristo. Siri hiyo hawakujulishwa wanadamu katika vizazi vingine; kama
walivyofunuliwa mitume wake watakatifu na manabii zamani hizi katika Roho; ya
kwamba Mataifa ni warithi pamoja nasi wa urithi mmoja, na wa mwili mmoja, na
washiriki pamoja nasi wa ahadi yake iliyo katika Kristo Yesu kwa njia ya Injili;
Injili hiyo ambayo nalifanywa mhudumu wake, kwa kadiri ya kipawa cha neema ya
Mungu niliyopewa kwa kadiri ya utendaji wa uweza wake.
Mimi,
niliye mdogo kuliko yeye aliye mdogo wa watakatifu wote, nalipewa neema hii ya
kuwahubiri Mataifa utajiri wake Kristo usiopimika; na kuwaangaza watu wote
wajue habari za madaraka ya siri hiyo, ambayo tangu zamani zote ilisitirika
katika Mungu aliyeviumba vitu vyote; ili sasa, kwa njia ya kanisa, hekima ya
Mungu iliyo ya namna nyingi ijulikane na falme na mamlaka katika ulimwengu war
oho; kwa kadiri ya kusudi la milele alilolikusudia katika Kristo Yesu Bwana
wetu. Katika yeye tunao ujasiri na uwezo wa kukaribia katika tumaini kwa njia
ya kumwamini.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Isa.
12:2 – 6 (K) 3
(K)
Kwa furaha mtateka maji katika visima vya wokovu.
Tazama,
Mungu ndiye wokovu wangu;
Nitatumaini
wala sitaogopa;
Maana
Bwana Yehova ni nguvu zangu
Na
wimbo wangu;
Naye
amekuwa wokovu wangu.
Basi,
kwa furaha mtateka maji
Katika
visima vya wokovu. (K)
Mshukuruni
Bwana, liitieni jina lake;
Yatangazeni
matendo yake kati ya mataifa,
Litajeni
jina lake kuwa limetukuka.
Mwimbieni
Bwana. (K)
Kwa
kuwa ametenda makuu,
Na
yajulikane haya katika dunia yote.
Paza
sauti, piga kelele, mwenyeji wa Sayuni;
Maana
Mtakatifu wa Israeli ni mkuu kati yako. (K)
SHANGILIO
Yn.
14:23
Aleluya,
aleluya,
Mtu
akinipenda, atalishika neno langu, na Baba yangu atampenda, na sisi tutakuja
kwake.
Aleluya.
INJILI
Lk.
12:39-48
Yesu
aliwaambia wanafunzi wake: Fahamuni neno hili, Kwamba mwenye nyumba angalijua
saa atakayokuja mwivi; angalikesha, wala asingaliacha nyumba yake kuvunjwa.
Nanyi jiwekeni tayari, kwa kuwa saa msiyodhani ndipo ajapo Mwana wa Adamu.
Petro
akamwambia, Bwana, mithali hiyo umetuambia sisi tu, au watu wote pia? Bwana
akasema, Ni nani, basi, aliye wakili mwaminifu, mwenye busara, ambaye bwana
wake atamweka juu ya utumishi wake wote, awape watu posho kwa wakati wake? Heri
mtumwa yule, ambaye bwana wake ajapo atamkuta anafanya hivyo. Kweli nawaambia,
atamweka juu ya vitu vyake vyote. Lakini, mtumwa yule akisema moyoni mwake,
Bwana wangu anakawia kuja, akaanza kuwapiga wajoli wake, wanaume kwa wanawake,
akila na kunywa na kulewa; bwana wake mtumwa huyo atakuja siku asiyodhani na
saa asiyojua, atamkata vipande viwili, na kumwekea fungu lake pamoja na
wasioamini.
Na
mtumwa yule aliyejua mapenzi ya bwana wake, asijiweke tayari, wala kuyatenda
mapenzi yake, atapigwa sana. Na yule asiyejua, naye amefanya yastahiliyo mapigo,
atapigwa kidogo. Na kila aliyepewa vingi, kwake huyo vitatakwa vingi; naye
waliyemwekea amana vitu vingi, kwake huyo watataka na zaidi.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment