MASOMO
YA MISA, OKTOBA 18, 2020
DOMINIKA
YA 29 MWAKA A
MWANZO:
Zab.
17:6,8
Ee
Mungu, nimekuita kwa maana utaitika, utege sikio lako ulisikie neno langu. Ee
Bwana, unilinde kama mboni ya jicho, unifiche chini ya uvuli wa mbawa zako.
________
SOMO
1
Isa.
45:1, 4-6
Haya
ndiyo Bwana amwambiayo Koreshi, masihi wake, ambaye nimemshika mkono wake wa
kuume, ili kutiisha mataifa mbele yake, nami nitalegeza viuno vya wafalme, ili
kufungua milango mbele yake, hata malango hayatafungwa. Kwa ajili ya Yakobo,
mtumishi wangu, na Israeli, mteule wangu, nimekuita kwa jina lako; nimekupa
jina la sifa; ijapokuwa hukunijua. Mimi ni Bwana, wala hapana mwingine; zaidi
yangu mimi hapana Mungu; nitakufunga mshipi ijapokuwa hukunijua; ili wapate
kujua toka maawio ya jua, na toka magharibi, ya kuwa hapana mwingine zaidi ya
mimi.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
________
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
96:1, 3-5, 7-10 (K) 7
(K)
Mpeni Bwana utukufu na nguvu.
Mwimbieni
Bwana wimbo mpya, Mwimbieni Bwana, nchi yote.
Wahubirini
mataifa habari za utukufu wake,
Na
watu wote habari za maajabu yake. (K)
Kwa
kuwa Bwana ni mkuu mwenye kusifiwa sana,
Na
wa kuhofiwa kuliko miungu yote.
Maana
miungu yote ya watu si kitu,
Lakini
Bwana ndiye aliyezifanya mbingu. (K)
Mpeni
Bwana enyi jamaa za watu,
Mpeni
Bwana utukufu na nguvu.
Mpeni
Bwana utukufu wa jina lake.
Leteni
sadaka mkaziingie nyua zake. (K)
Mwabuduni
Bwana kwa uzuri wa utakatifu,
Tetemekeni
mbele zake, nchi yote.
Semeni
katika mataifa, Mungu ni mfalme,
Atawahukumu
watu kwa adili. (K)
________
SOMO
2
1Thes.
1:1-5
Paulo,
na Silwano, na Timotheo, kwa kanisa la Wathesalonike, lililo katika Mungu Baba,
na katika Bwana Yesu Kristo. Neema na iwe kwenu na amani.
Twamshukuru
Mungu sikuzote kwa ajili yenu nyote, tukiwataja katika maombi yetu. Wala
hatukuachi kuikumbuka kazi yenu ya imani, na taabu yenu ya upendo, na saburi
yenu ya tumaini lililo katika Bwana wetu Yesu Kritu, mbele za Mungu Baba yetu.
Kwa maana, ndugu mnaopendwa na Mungu, twajua uteule wenu; ya kwamba injili yetu
haikuwafikia katika maneno tu, bali na katika nguvu, na katika Roho Mtakatifu,
na uthibitifu mwingi.
________
SHANGILIO
Yn.
15:15
Aleluya,
aleluya,
Ninyi
nimewaita rafiki, kwa kuwa yote niliyoyasikia, kwa Baba yangu nimewaarifu.
Aleluya.
________
INJILI
Mt.
22:15-21
Mafarisayo
walienda zao, wakafanya shauri, jinsi ya kumtega Yesu kwa maneno. Wakatuma
kwake wanafunzi wao pamoja na Maherodi, wakasema, Mwalimu, twajua ya kuwa wewe
u mtu wa kweli, na njia ya Mungu waifundisha katika kweli, wala hujali cheo cha
mtu awaye yote, kwa maana hutazami sura za watu. Basi utuambie, Waonaje? Ni
halali kumpa Kaisari kodi, ama sivyo? Lakini Yesu akaufahamu uovu wao, akasema,
Mbona mnanijaribu, enyi wanafiki? Nionyesheni fedha na kodi. Nao wakamletea
dinari. Akawaambia, Ni ya nani sanamu hii, na anwani hii? Wakamwambia, Ni ya
Kaisari. Akawaambia, Basi, mlipeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na Mungu yaliyo
ya Mungu.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment