“MBEGU
ZA UZIMA”
Tafakari
ya kila siku
Jumapili,
Oktoba 18, 2020.
Dominika
ya 29 ya Mwaka
SIKU
YA UMISIONARI ULIMWENGUNI
Isa
45:1, 4-6;
Zab 95: 1, 3-5, 7-10;
1
Thes 1:1-5;
Mt
22:15-21
UMISIONARI
KATIKA MOYO WA IMANI YA KIKRISTO!
Muktasari
wa masomo yetu
(Isaya
45:1.4-6). Kurudi kwa wana Waisraeli kutoka utumwani chini ya mfalme Cyrus
haionekani tu kama alama ya huruma ya Mungu kwa watu wake bali kama alama ya
Mungu kuwa Bwana wa wote.
(1 Thessalonike 1:1-5). Hapa
linabeba taarifa za kwanza za Paulo kwa Wakristo wa Thesalonike. Nia yake
inaonekana kila mahali.
(Mathayo 22:15-21). Katika hali
ya kutaka kumtega Yesu aseme kitu ambacho kinaleta utengano, maadui wake
wanamuuliza kama ni halali kulipa kodi kwa Kaisari au la?
Ulishawahi
kujiuliza mtu anavyokuwa Mkristo, “kwanini Mungu asimpeleka tu Mbinguni?” jibu,
ni kwamba Mungu anampango na kila mmoja wetu, umeumbwa ili utimize sehemu ya
umisionari wako. Na umisionari uanaanza na maneno ya Yesu, Mathayo 4:18 “njoo
nifuate mimi nitakufanya kuwa mvuvi wa watu”. Ni ishara wazi kwamba Yesu
alivyokuwa anamuita mtu alikuwa hamuiti kuja kuishi maisha naye bila kazi, bali
kwa maisha yaliojikita katika umisionari. Hakuwaita kwenda hekaluni, au kwenye
Tora, bali maisha ya ufuasi uliotukuka. Katika Matendo ya Mitume 1:8 tunaona
kwamba kabla ya Yesu kupaa aliwaita mitume wake akawaambia kwamba wao watakuwa
mashahidi wake kuanzia Yerusalemu, Yudea, Samaria na miisho ya ulimwengu. Na
katika matendo ya Mitume 2, Roho Mtakatifu alitolewaa kama zawadi kwa watu ili
waweze kutangaza neno la Mungu ulimweuni kote. Tangu Pentekoste utume wa Mungu
umekuwa ukiendelea kokote ulimwenguni. Utume huu unaenda kila mahali ukiwa
unamuweka Yesu katikati. Utume ni kitu ambacho tunaitwa kila mmoja tuweze
kushiriki zaidi na zaidi. Utume ni kutoa ushuhuda kuhusu Yesu kwa kile tunacho
kiamini hasa kumpenda Mungu na jirani.
Mungu
wa Biblia sio Mungu wa utengano. Yeye anatusafisha sisi kwanza na baadae
anatutumia sisi tuweze kuusafisha ulimwengu. Hii daima imekuwa ndio njia ya
Mungu. Wakati Mungu anavyotaka kubadilisha ulimwengu alimchagua Noah afanye
kitu ambacho hajawahi kufanya kabla(kutengeneza safina) ili afanya ambacho
hajawahi kufanya kabla (mvua). Wakati Mungu alivyotaka kuleta mabadiliko
alimuita Abrahamu aache nchi yake mwenyewe. Wakati Mungu alivyotaka kuwaokoa
waisraeli Misri alimchagua mtu mmoja ambaye alikuwa sio muongeaji sana, Musa na
kumtuma kwa Farao. Wakati Mungu alivyo hitaji mtu wakuficha wapelelezi wa
Jeriko, alimchagua Rahabu (kahaba). Wakati Mungu alivyotaka kumuua Goliathi
alimchagua kijana mmoja mchungaji tu naye ni Daudi. Wakati Mungu alivyotaka
kuwakoa wana Waisraeli waliobaki utumwani Babuloni alimchagua mshichana mdogo
tu Ester.
Wakati
Yesu alivyotaka kuwachagua wafuasi wake aliwachagua watu wa chini wavuvi na
watoza ushuru, tena muongeaji sana Petro na wana wawili wa ngurumo akawaambia
waache neti zao wamfuate. Shuhuda ni mtu ambaye anasema tu kile alichoona na
kukishuhudia. Ndio hivyo. Wewe ni mtaalamu wa maisha yako. Unacho takiwa ni
kushirikisha kile ambacho Mungu amefanya katika maisha yako. Sisi wote
tumeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu.
Barua
ya Mt.; Pailo kwa Wathesalonike inahitaji uangalifu mkubwa “Maneno yetu ya
Injili sio maneno matupu bali ni Nguvu”. Habari njema kama alivyo ihubiri kwa
hawa wa Giriki kabla hawajafanya ugumu wa mioyo yao, kwanza lilipo pokelewa na
likazama katika udongo mzuri na kuleta matumaini makubwa. Kwa njia ya Roho
Mtakatifu aliyekuwa ndani ya Paulo na wale wote waliompokea, injili ya Kristo
ilipata umwilisho katika maisha yao. Je, hivi sivyo tunayo tamani hali iweze
kuwa kila mahali?
Je,
sisi ni wapi tunapaswa kushirikisha habari hii njema,? Je huu si utume usio
wezekana? Ni utume usiokwepeka. Tunaanzia wapi? Pale pale tunapoishi. Katika
Yerusalemu yetu, kwa marafiki zako, kwa wafanyakazi wenzako, jirani, na watu
wote walio karibu yako. Na hii ndio sehemu ya pili ya kufanya hilo, sio tu kwa
walio katika Yerusalemu yangu, kuwaambia kuhusu habari njeama ya Kristo, tuna
sehemu tunapaswa kwenda mbali kabisa na mazingira yetu , watu tofauti na
tamaduni zako mwenyewe, mazingara yako, watu walio karibu nasi lakini waliotoka
mazingira tofauti na yetu. Paulo anasema “Nimekuwa yote kwa watu wote, ili kwa
njia moja niwaokoe wengine” (1Kor 9:22)
Sala:
Bwana, nipo hapa nitume mimi. Nitume mimi niweze kuwa shuhuda wako. Amina
Muktasari
wa “UJUMBE WA BABA MTAKATIFU FRANSISKO KWA SIKU YA UMISIONARI ULIMWENGUNI 2020”
Kanisa
kwa asili ni la Kimisionari, hivyo ni vizuri kujiuliza baadhi ya maswali kuhusu
kitambulisho chetu sha ukristo, na majukumu yetu kama Waamini katika ulimwengu
uliochanganikiwa, uliojaa kukata tamaa na ulimwengu uliokumbwa na vita na
kuharibikiwa na kulenga kuwaharibu wale wasio na hatia. Nini msingi wa utume
wetu? Nini kiini cha utume wetu? Ni vitu ghani muhimu tunapaswa kubeba tunavyo
fanya utume wetu?
Utume
na nguvu ya kubadilisha ya Injili ya Kristo, Njia, Ukweli na Uzima
• Utume wa kanisa uliolengwa kwa
watu wote wenye mapenzi mema na wasio na mapenzi mema, unajikita katika nguvu
ya kubadilisha ya Injili. Injili ni habari njama iliojaa furaha ya kubadilisha,
kwani inabeba maisha mapya. Maisha hayo yanatuweka huru kutoka katika ubinafsi,
na ni chanzo cha chemichem ya upendo.
• Kwa njia ya utume huu wa Kanisa
Yesu mwenyewe anaendelea kuhubiri, utume wake unaweka katika zama zetu wakati
ule wa historia wakati Yesu alivyokuwa anahubiri mwenyewe na hivyo kutangaza
wokovu. Kwa njia ya kutangaza Injili, Yesu mfufuka anawekwa hai katika wakati
wetu.
• Injili ni mtu ambaye anajitoa
mwenyewe kila mara na kuwaalika wengine kumpokea Kristo kwa unyenyekevu na kwa
Imani kushiriki maisha yake kwa kujiingiza katika mafumbo ya masha ya Kristo,
mateso, Kifo na ufufuko.
• Ulimwengu unahitaji sana Injili
ya Yesu Kristo. Kwa njia ya Injili Kanisa linaendelea na kazi yake ya kuwa
Msamaria mwema, kwa kuponya vidonda vinavyo toa damu vya wanadamu, kama
mchungaji mwema, na kuwaongoza wote wanao hangaika na kupita njia ambayo
haiwezi kuwapeleka mahali.
• Utume wa Kanisa unangarishwa kwa
njia ya safari ya kiroho. “Tunaitwa kutoka katika maeneo yetu wenyewe na kutoka
njee ili tuweze kukutana na wale walio mbali na mwanga wa Injili” (Evangelii
Gaudium, 20).
• Utume unalionesha kanisa kwamba
lenyewe sio mwisho, bali ni chombo cha kupeleka ufalme.
• Vijana ndio matumaini ya utume.
Nafsi ya Yesu na Injili aliyo hubiri imeendelea kugusa mioyo na kuwavutia
vijana. Wanatafuta njia ya nguvu ya kujiweka wenyewe katika kuwahudumia
wanadamu. Mkutano wa Maaskofu ambao utakuwa mwaka 2018, wenye maada ya “vijana,
Imani na mangamuzi katika wito”, inatoa nafasi kwa vijana kujiingiza katika
umisionari ambao unahitaji utajiri wao na ubunifu wao.
• Jamii ya utume ya Kipapa ni njia
nzuri za kuwaamsha kila jumuiya ya Kikristo kutamani kwenda zaidi ya mipaka yao
na kutangaza Injili kwa wote.
• Siku ya Umisionari duniani,
ambayo inatangazwa na Jamii ya kueneza Imani, ni nafasi nzuri ya kuwezesha moyo
wa kimisionari katika jamaa za Kikristo kuunganika katika sala, ushuhuda wa
maisha na muunganiko wa matendo mema, katika kuitika kwa hali zote na kuhubiri.
• Sisi tuvutwe na mfano wa Maria,
Mama wa habari njema. Kwa kuvutwa na Roho Mtakatifu, alikaribisha neno la uzima
ndani ya moyo wake kwa Imani nyenyekevu. Tunamuomba Mama Maria atuombee tuweze
kusema “ndio”, kwa ufahamu wote na kufanya neno la Yesu liweze kuwa hai wakati
wetu. Tunamuomba atuombee tuweze kuwa na hali mpya ndani yetu ya kuhubiri habari njema ya maisha.
Tunamuomba yeye atuombee tuweze kuwa watakatifu tuweze kutambua njia mpya za
kuleta zawadi ya ukombozi kwa waume na wake.
------------------------
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment