“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari
ya kila siku
Jumamosi,
Oktoba 17, 2020,
Juma
la 28 la Mwaka wa Kanisa
Ef
1: 15-23;
Zab
8: 2-7;
Lk
12: 8-12.
IMANI
ILIYO JARIBIWA!
Karibuni
ndugu zangu kwa adhimisho la Misa Takatifu asubuhi ya leo. Leo basi Paulo
anaandika sehemu ya barua ya kwa Waefeso panapotoka somo letu la kwanza leo
katika lugha ya utulivu kabisa na matumaini. Anamshukuru Mungu jinsi Waefeso
walivyomuweka Mungu mbele na anawombea, na anazidi kuwaeleza juu ya nguvu ya
Kristo na jinsi alivyoviweka vitu vyote chini ya miguu yake.
Inamlazimu
Paulo atoe maelezo marefu juu ya nguvu ya ukuu wa Kristo kwa sababu Waefeso
waliishi katika jumuiya waliposhambuliwa na Filosofia na nguvu nyingine za
kisiri. Paulo anawatia moyo kwamba Kristo ananguvu na ndiye wa kutumainiwa.
Jibu
la namna hii tunalihitaji kwa nyakati zetu hizi pia. Wengi wetu tunashindwa
kuziona nguvu za Kristo; Kristo ni rasilimali kubwa sana. Wengi wetu tumerudi
nyuma kwa sababu tunamuona Kristo kana kwamba hatoshi; tuombe kuwa na imani
zaidi. Kristo anatosha.
Katika
injili Yesu anasema kwamba anayemkana mbele ya watu naye pia atamkana mbele ya
Babaye. Tunamkana Kristo pale tunapomuona kana kwamba hatoshi maishani mwetu.
Kila siku tunamkana Kristo kwa pale tunapoona aibu kusali mbele za watu au pale
tunapowaona kama washamba wale wanaopendelea masuala ya kiroho. Tunawaona
washamba. Mtu akivaa rozari anaonekana kwa baadhi ya watu kama ni mshamba zaidi
ya yule aliyevaa licheni la dhahabu lililochorwa labda mnyama. Huyu aliyevaa
hili licheni tunamuona kuwa mjanja zaidi. Hapa ni kumkana Kristo hadharani.
Au
kwa pale unakuta mabaa au viwanja vya mipira vimejaa kuliko kanisa. Hapa ni
kumkana Kristo hadharani. Au kukuta kwamba watu wanaovaa nguo panapana na za
heshima tunawaona kama waliorudi nyuma zaidi ya wale wanaovaa vimodo vyembamba
na vyakubana. Hapa ni kumpatia shetani nguvu na kumdidimiza Kristo.
Tuache
kumdidimiza Kristo ndugu zangu.
Kama
wimbo wetu wa katikati unavyotuongoza leo, tutambue kwamba Mungu anapaswa
kusifika na vinywa vya watoto na wote; tumpatie muda na kumtagaza. Macho yangu
yanapoona ya kishetani zaidi kuliko ya kimungu ni dhahiri kwamba ninamkana
Kristo hadharani. Tumweke Kristo mbele.
Yesu
katika injili anasema tusiogope kwa pale tupelekwapo mikononi mwa maadui zetu.
Kila mmoja wetu aondoe aibu na hofu inayomzuia asiwe chombo kiteule cha Kristo
kinachomshuhudia. Amina.
------------------------
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment