MASOMO
YA MISA, OCTOBA 17, 2020
JUMAMOSI,
JUMA LA 28 LA MWAKA
SOMO
LA 1
Efe
1:15-23
Tangu
nilipopata habari za Imani yenu katika bwana Yesu, na pendo lenu kwa watakatifu
wote, siachi kutoa shukrani kwa ajili yenu; nikiwakumbuka katika sala zangu,
Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu awape ninyi roho wa hekima na
ya ufunuo katika kumjua yeye; macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, tumjue tumaini
la mwito wake jinsi lilivyo ;na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika
watakatifu jinsi ulivyo.
Kwa
kadiri ya utendaji wa nguvu za uweza wake;ulipotenda katika kristo alipomfufua
katika wafu,akamwekea mkono wake wa kuume katika ulimwngu wa roho ; juu sana
katika ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani na kila jina litajwalo
wala si ulimwenguni humu tu bali katika ule ujao pia akavitia vitu vyote chini
ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa;
ambalo ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote.
Hilo
ndilo neno la Bwana... Tumshukuru Mungu
WIMBO
WA KATIKATI
Zab
8:1-6 (K) 6
(K)
Umemtawaza mwanao juu ya kazi za mikono yako
Wewe
Mungu Bwana wetu,
Jinsi
lilivyo tukufu jina lako duniani mwote!
Wewe
umeuweka utukufu wako mbinguni;
Vinywani
mwa watoto wachanga na wanyonyao. (K)
Nikiziangalia
mbingu zako, Kazi ya vidole vyako,
Mwezi
na nyota ulizoziratibisha,
Mtu
ni kitu gani hat umkumbuke
Na
binadamu hata umwangalie. (K)
Umemfanya
mdogo punde kuliko Mungu;
Umemvika
taji ya utukufu na heshima
Umemtawaza
juu ya kazi za mikono yako
Umevitia
vitu vyote chini ya miguu yake. (K)
SHANGILIO
Mt
11:35
Aleluya,
Aleluya
Nakushukuru
baba Bwana wa mbingu na nchi
Kwa
kuwa mambo haya uliyaficha
Wenye
hekima na akili
Ukawafunulia
watoto wachanga
Aleluya.
INJILI
Lk.
12:8-12
Yesu
aliwaambia wanafunzi wake: Nami nawaambia, kila atakayenikiri mbele ya watu,
Mwana wa Adamu naye atamkiri yeye mbele ya malaika wa Mungu; na mwenye kunikana
mbele ya watu, huyo atakanwa mbele ya malaika wa Mungu.
Na
kila mtu atakayenena neno juu ya Mwana wa Adamu atasamehewa, bali aliyemkufura
Roho Mtakatifu hatasamehewa.
Na
watakapowapeleka ninyi mbele ya masinagogi na maliwali na wenye mamlaka,
msifadhaike kwa kuwaza maneno yenu jinsi mtakavyojibu au kusema; kwa kuwa Roho
Mtakatifu atawafundisha saa ile ile yawapasayo kuyasema.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment