“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Ijumaa,
Oktoba, 23, 2020,
Juma
la 29 la Mwaka wa Kanisa
Ef
4:1-6;
Zab
23:1-6;
Lk
12:54-59
KUFAFANUA
ALAMA ZA NYAKATI ZETU!
Karibuni
ndugu zangu kwa adhimisho la Misa Takatifu asubuhi ya leo. Leo tafakari yetu
inaanza kwa kuiangalia zaburi yetu ya wimbo wa katikati ambapo tunakutana na
zaburi yetu ikisitizia miongoni mwa mengine-juu ya mtu atakayeweza kupanda
mlima wa Mungu. Inasema ni yule aliyena mikono safi asiyedhulumu.
Katika
Biblia, Abrahamu, Musa na Elia ni miongoni mwa waliopanda mlima Mtakatifu wa
Mungu na huko basi waliweza kukutana na Bwana na kuongea naye. Na kweli
hawakuwa na mioyo ya kunyanyasa yeyote yule.
Huu
ndio ujumbe ambao Paulo anawaachia wale Wakristo Waefeso leo kwamba nao basi
wawe na moyo kama huu ili waupande mlima wa Bwana. Wasaidiane, wabebeane mizigo
yao, kwa kujitolea, ukarimu na uvumilivu.
Huu
ndio wito wetu kama wakristo. Hizi ndizo tunu tunazoalikwa kuzifufua kila kukicha
kama wakristo. Wakristo tuzidishe uvumilivu na kujitolea. Uvumilivu na
kujitolea umekosekana ndani ya jumuiya yetu siku hizi. Kila mmoja anatafuta
chake, wengi wanaachwa bila matunzo kwa kukosekana watu wanaojitolea. Wengi
wetu ni maskini siku hizi kwa sababu idadi kubwa hatujitolei. Tunahitaji watu
wa kujitolea; tuijenge jumuiya yetu. Wengi wameshindwa kusoma au kupata ujuzi
wowote kwa kukosekana wa kujitolea. Tunahitaji watu wenye kujitolea zaidi.
Katika
injili Yesu anawaeleza makutano kwamba wao ni wataalamu sana kwa mambo ya
kidunia, wanajua kutabiri mengi yahusuyo dunia lakini kuhusu nyakati za mwisho
hawajui namna ya kuzitabiri. Yote haya yanatokea kwa sababu waliyatupa mambo
haya ya Kimungu pembeni na wakaishia kutokujua zaidi juu ya nyakati za mwisho.
Hii
itupatie changamoto hasa sisi tulio na ujuzi au kisomo fulani. Mara nyingi
unakuta watu tunaujuzi fulani, tunajua biashara, mahesabu, kemia, kuendesha
gari vizuri, kupasua watu kama daktari mzuri lakini inapotokea mambo ya Kimungu
tupo hewa. Tubadilike, tujihusishe na mambo ya Kimungu, tusitumie muda wote kwa
ajili ya mambo ya hapahapa tu duniani bila kutenga muda kwa ajili ya mambo ya
Kimungu.
Kila
mwenye ujuzi aangalie asitumie muda wote kwenye huo ujuzi wake. Aache pia muda
kwa ajiili ya kuongea na Mungu ili basi amfundishe juu ya nyakati zijazo;
atufundishe namna ya kutabiri majira na nyakati. Tusibakie wajinga
------------------------
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment