MASOMO
YA MISA, OKTOBA 23, 2020
IJUMAA,
JUMA LA 29 LA MWAKA WA KANISA
SOMO
1
Efe.
4:1 – 6
Nawasihi,
mimi niliye mfungwa katika Bwana, mwenende kama inavyoustahili wito wenu
mlioitiwa; kwa unyenyekevu wote na upole, kwa uvumilivu, mkichukuliana katika
upendo; na kujitahidi kuuhifadhi umoja wa Roho katia kifungo cha amani. Mwili
mmoja, na Roho mmoja, kama na mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu.
Bwana mmoja, Imani moja, ubatizo mmoja. Mungu mmoja, naye ni Baba wa wote,
aliye juu ya yote na katika yote na ndani ya yote.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
24:1 – 6 (K) 6
(K)
Hiki ndicho kizazi cha wakutafutao, Ee Bwana.
Nchi
na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana,
Dunia
na wote wakaao ndani yake.
Maana
ameiweka misingi yake juu ya bahari,
Na
juu ya mito ya maji aliithibitisha. (K)
Ni
nani atakayepanda katika mlima wa Bwana?
Ni
nani atakayesimama katika patakatifu pake?
Mtu
aliye na mikono safi na moyo mweupe,
Asiyeiinua
nafsi yake kwa ubatili,
Wala
hakuapa kwa hila. (K)
Atapokea
Baraka kwa Bwana,
Na
haki kwa Mungu wa wokovu wake.
Hiki
ndicho kizazi cha wamtafutao,
Wakutafutao
uso wako, Ee Mungu wa Yakobo. (K)
SHANGILIO
Efe.
1:17, 18
Aleluya,
aleluya,
Mungu
wa Bwana wetu Yesu Kristo, awape roho ya hekima mjue tumaini la mwito wake.
Aleluya.
INJILI
Lk.
12:54-59
Yesu
aliwaambia makutano pia, kila mwonapo wingu likizuka pande za magharibi mara
husema, Mvua inakuja; ikawa hivyo. Na kila ivumapo kaskazi, husema, Kutakuwa na
joto; na ndivyo ilivyo. Enyi wanafiki, mwajua kuutambua uso wa nchi na mbingu;
imekuwaje, basi, kuwa hamjui kutambua majira haya?
Na
mbona ninyi wenyewe kwa nafsi zenu hamwamui yaliyo haki? Maana, unapofuatana na
mshitaki wako kwenda kwa mwamuzi, hapo njiani fanya bidi kupatanishwa naye,
asije akakuburuta mpaka mbele ya kadhi; yule kadhi akakutia mikononi mwake
mwenye kulipiza, na yule mwenye kulipiza akakutupa gerezani. Nakuambia, Hutoki
humo kamwe hata uishe kulipa senti ya mwisho.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment