ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari
ya kila siku
Jumanne,
Agosti 12, 2025
Juma
la 19 la Mwaka wa Kanisa
Kum:
31:1-8
Zab
147: 12-20
Mt
18: 1-5, 10, 12-14
NI
NANI MKUBWA KATIKA UFALME WA MUNGU?
Kuna
video katika mitandao inayohusu Matt Woodrum, ambayo inabeba jina la “Kijana
mlemavu awavutia wengi nyakati za mwisho”. Huyu kijana Matt ilikuwa vigumu
kwake kutembea, lakini alishiriki katika mashindano ya kukimbia (katika
mzunguko wa duara). Wakati mashindano yalipoanza wakimbiaji wote walimpita
nakukimbia nakumaliza. Wakati akiwa nusu ya mzunguko wale wakimbiaji wengine
walishamaliza mzunguko mwingine nakumpita. Na wakati hajamaliza mzunguko wa
kwanza wote wakamaliza mizunguko yote. Lakini Matt hakuacha kuendelea
kuzunguka, hata yule kiongozi wake alivyomwambia aache yeye hakuacha. Alisema
anataka kumaliza. Hakujali ni sehemu ghani yeye alitaka kumaliza. Watu kwakuona
moyo wake, wakamzunguka na kuanza kumpigia makofi nakusema “songa mbele, songa
mbele Matt” Matt aliwafundisha wote somo. “Kushinda haimaanishi kumaliza kwa mwendo
uliopangwa”
Katika
somo la Injili tunaona wafuasi wa Yesu wakimuuliza; ‘ni nani aliyemkubwa katika
Ufalme wa mbinguni?’ Matt, anatupa jibu, yule mdogo, mnyonge, anayeonewa,
aliyekama mtoto, asiyejiweza………Wale waliojawa na elimu ya juu kabisa, matajiri
na wenye mamlaka, wakialikwa kwenye sherehe kwanza wanaangalia ni nani
atakuwepo ili kusimamia shughuli zake? Pia nitakuwa katika sehemu ghani kati ya
waalikwa? Je nitapewa heshima ghani? Wakati kama mtoto, au mlemavu angealikwa
kwa sherehe hiyo, angejisikia mwenye bahati sana kualikwa kwenye sherehe kama
hiyo. Wanatambua kwakweli hawastahili kwa mwaliko huo, lakini wamealikwa na
Bwana wa sherehe.
Wafuasi
nao wameanguka kwenye mtego wakudhani kwamba wanastahili kwenye Ufalme wa
Mungu. Kwamba ni haki yao kuwa pale, na kuwa katika nafasi ya juu kabisa.
Wakati watoto hawajui hata kama watashiriki katika Ufalme huo. Wafuasi walikosa
unyenyekevu, walipoteza maana ya maisha yao nakujisahau wao ni nani. Je, mimi
na wewe tupo je? Je, unafikiri una haki ya kuwa katika Ufalme wa Mbinguni? Je,
unasubiria sehemu ya juu kwasababu ya utume unaofanya kwaajili ya Mungu? Kama
unataka kuingia katika Ufalme wa Mungu, kuwa na moyo mnyofu kama wa watoto.
Tunapaswa kuwa na moyo mnyofu uliojaa unyenyekevu ili tuyapokee vyema mapenzi
ya Mungu, kwa namna hii bila hata mastahili yetu, twajuaje kama Mungu
hatatukaribisha kwake? Daima tuombee neema hiyo.
Sala:
Bwana, fanya moyo wangu uwe mnyenyekevu na mnyoofu kama wako. Amina.
🙏🏽
ReplyDelete