MASOMO YA MISA
- AGOSTI 12, 2025
JUMANNE YA 19 YA MWAKA
SOMO 1
Kum 31: 1-8
Musa alienda akawaambia Waisraeli maneno haya yote.
Akawaambia, Mimi leo ni mwenye miaka mia na ishirini; siwezi tena kutoka na
kuingia, na Bwana ameniambia, Hutavuka mto huu Yordani. Bwana, Mungu wako,
ndiye atakayevuka mbele yako, atawaangamiza mataifa haya mbele yako, nawe
utawamiliki; na Yoshua atavuka mbele yako, kama Bwana alivyonena. Na Bwana
atawatenda hao kama vile alivyowatenda Sihoni na Ogu, wafalme wa Waamori, na
nchi yao, ambao aliwaharibu. Nave Bwana atawatia mikononi mwenu, nanvi
mtawatenda kadiri ya amri ile niliyowaamuru. Iweni hodari na moyo wa ushujaa,
msiogope wala msiwahofu; kwa maana Bwana, Mungu wako, yeye ndiye anayekwenda
pamoja nawe, hatakupungukia wala kukuacha.
Musa akamwita Yoshua, akamwambia machoni pa Israeli wote,
Uwe hodari na moyo wa ushujaa, maana utakwenda pamoja na watu hawa hata nchi
Bwana aliyowaapia baba zao, ya kwamba atawapa; nawe utawarithisha. Naye Bwana,
yeye ndiye atakayekutangulia, atakuwa pamoja nawe, hatakupungukia wala
kukuacha; usiogope wala usifadhaike.
Neno la Bwana...Tumshukuru
Mungu
WIMBO WA KATIKATI
Kum. 32 :3-4, 7-9, 12 (K) 9
(K) Sehemu ya Bwana ni watu wake.
Nitalitangaza Jina la Bwana;
Mpcni ukuu Mungu wetu.
Yeye Mwamba, kazi yake ni kamilifu;
Maana, njia zake zote ni haki.
Mungu wa uaminifu, asiye na uovu,
Yeye ndiye mwenye haki na adili. (K)
Kumbuka siku za kale,
Tafakari miaka ya vizazi vingi;
Mwulize baba yako, naye atakuonyesha;
Wazee wako, nao watakuambia. (K)
Yeye Aliye Juu alipowapa mataifa urithi wao,
Alipowabagua wanadamu,
Aliweka mipaka ya watu
Kwa kadiri ya hesabu ya wana wa Israeli.
Maana, sehemu ya Bwana ni watu wake,
Yakobo ni kura ya urithi wake. (K)
Bwana peke yake alimwongoza,
Wala hapakuwa na mungu mgeni pamoja naye. (K)
SHANGILIO
Yn 15: 15
Aleluya, aleluya,
Bwana anasema: Siwaiti tena watumwa, lakini ninyi
nimcwaita rafiki, kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba yangu, nimewaarifu.
Aleluya.
INJILI
Mt. 18: 1-5, 10, 12,1 4
Wanafunzi walimwendea Yesu wakisema, Ni nani basi aliye
mkuu katika ufalme wa mbinguni? Akaita mtoto mmoja, akamweka katikati yao,
akasema, Amin, nawaambia, Msipoongoka na kuwa kama vitoto, hamtaingia kamwe
katika ufalme wa mbinguni.
Basi, ye yote ajinyenyekeshaye mwenyewe kama mtoto huyu,
huyo ndiye aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni.
Na ye yote atakayempokea mtoto mmoja mfano wa huyu kwa
jina langu, anipokea mimi.
Angalieni msidharau mmojawapo wadogo hawa; kwa maana
nawaambia ya kwamba malaika zao mbinguni sikuzote huutazama uso wa Baba yangu
aliye mbinguni.
Mwaonaje? mtu akiwa na kondoo mia, mmoja akampotea, je!
hawaachi wale tisa na tisini, akaenda milimani, na kumtafuta yule aliyepotea?
Vivyo hivyo haipendezi mbele za Baba yenu aliye mbinguni kwamba mmoja wa wadogo
hawa apotee.
Neno la Bwana...Sifa kwako, ee Kristo
No comments:
Post a Comment