MASOMO YA MISA, MEI 6, 2023
JUMAMOSI, JUMA LA 4 LA PASAKA
SOMO 1
Mdo. 13:44-52
Paulo na wenziwe wakaingia katika sinagogi siku
ya sabato, wakaketi. Watu wengi, karibu mji waote, wakakusanyika walisikie neno
la Mungu. Bali Wayahudi walipowaona makutano, wakajaa wivu, wakayakanusha
maneno yaliyonenwa na Paulo, wakibisha na kutukana. Paulo na Barnaba wakanena
kwa ushujaa wakasema, Ilikuwa lazima neno la Mungu linenwe kwenu kwanza; lakini
kwa kuwa mnalisukumia mbali, na kujiona nafsi zenu kuwa hamkustahili uzima wa
mille, angalieni, twawageukia Mataifa. Kwa sababu ndivyo tulivyoamriwa na
Bwana,
Nimekuweka uwe nuru ya Mataifa, upate kuwa
wokovu hata mwisho wa dunia.Mataifa waliposikia hayo wakafurahi,
wakalitukuza neno la Bwana, nao waliokuwa wamekusudiwa uzima wa milele
wakaamini. Neno la Bwana likaenea katika nchi ile yote.
Lakini Wayahudi wakawafitinisha wanawake watauwa
wenye cheo na wakuu wa mji, wakawataharakisha watu wawaudhi Paulo na Barnaba;
wakawatoa katika mipaka yao. Nao wakawakung’utia mavumbi ya miguu yao, wakaenda
Ikonio. Na wanafunzi walijaa furaha na Roho Mtakatifu.
Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 98:1-4 (K) 3
(K) Miisho yote ya dunia imeuona Wokovo wa Mungu
wetu.
Au: Aleluya.
Mwimbieni Bwana wimbo mpya,
Kwa maana ametenda mambo ya ajabu.
Mkono wa kuume wake mwenyewe,
Mkono wake mtakatifu umemtendea wokovu. (K)
Machoni pa mataifa ameidhihirisha haki yake.
Amezikumbuka rehema zake,
Na uaminifu wake kwa nyumba ya Israeli. (K)
Miisho yote ya dunia imeuona
Wokovu wa Mungu wetu.
Mshangilieni Bwana, nchi yote,
Inueni sauti, imbeni kwa furaha, imbeni zaburi.
(K)
SHANGILIO
Rum. 6:9
Aleluya, aleluya.
Kristo akiisha kufufuka katika wafu, hafi tena
wala mauti haimtawali tena.
Aleluya.
INJILI
Yn. 14:7-14
Yesu aliwambia wanafunzi wake: Kama mngalinijua
mimi, mngalimjua na Baba, tangu sasa mnamjua, tena mmemwona.
Filipo akamwambia, Bwana, utuonyeshe Baba,
yatutosha.
Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi
siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona mimi amemwona Baba; basi wewe
wasemaje, Utuonyeshe Baba? Husadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu
ndani yangu? Hayo maneno niwaambiayo mimi siyasemi kwa shauri langu; lakini
Baba akaaye ndani yangu huzifanya kazi zake. Minisadiki ya kwamba mimi ni ndani
ya Baba, na Baba yu ndani yangu; la! Hamsadiki hivyo, sadikini kwa sababu ya
kazi zenyewe. Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo
mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi
naenda kwa Baba. Nanyi mkiomba lolote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili
Baba atukuzwe ndani ya Mwana. Mkiniomba neno lolote kwa jina langu,
nitalifanya.
Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
Copyright © 2023, "MASOMO YA MISA"
published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania. Readings reproduced by
Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com
No comments:
Post a Comment