Tafakari ya Pasaka
Jumamosi, Mei 2, 2026
Juma la 4 la Pasaka
Mdo 13:44-52;
Zab 98:1-4 (R. 3);
Yn 14:7-14.
MUNGU KUDHIHIRIKA NDANI YA MAISHA YETU!
Mara nyingi, hatujui ni kwa jinsi ghani Mungu anajifunua
mwenyewe katika maisha yetu kama Filipo, anayetaka kumuona Baba. Alikuwa mbele
ya Yesu, na bado anamtafuta Mungu. Sisi pia katika maisha yetu. Mungu yupo nasi
daima lakini kwasababu ya mawazo yetu na mitizamo yetu tunamtafuta. Sisi nasi
tunamtafuta Mungu na baadae tuna mtambua Yesu mbele yetu.
Paulo na Baranabas walitambua utambulisho wa kweli wa
Yesu na wanamhubiri kwa ujasiri mkubwa, kwa mataifa licha ya mateso na
vipingamizi. Kama sisi tunajiita wakristo, Kristo anapaswa kudhihirika katika
maisha yetu. Kama kumuona Yesu ni kumuona Mungu Baba ni wazi kwa matumaini na
katika sala, kutuona sisi ni kumuona Yesu pia.
Injili ya Yohane inatumia lugha hii mara nyingi kuonesha
umoja mkamilifu wa Yesu na Baba yake. Ni jambo zuri namna ghani sisi nasi
kusema sisi hatuseme wenyewe bali ni Kristo anasema ndani yetu? Hili ndilo
linalopaswa kuwa lengo letu la kila mara. Kama tutaongea maneno kwa wengine,
tukiwa tumejikita katika hekima yetu wenyewe na uelewa wetu wenyewe, ni lazima
tuji nyenyekeshe na kutambua kwamba maneno yetu hayawezi kuwa na nguvu. Lakini
kwa upande mwingine, lakini kama tunaweza kusema maneno yaliyo jaa Kristo,
maneno ambayo yanasemwa kutoka ndani ya moyo wake, tutaanza kuona maneno hayo
yanakuwa na manufaa katika maisha ya watu. Maneno yana maana sana, na tunapaswa
kuwa makini katika kuongea na kuwa na ujasiri na kile tunachosema, jinsi ya
kusema na tunasemaje. Kumruhusu Baba aongee ndani mwetu na kupitia sisi maneno
yetu yanakuwa na ujasiri na nguvu. Yanakuwa maneno ambayo Mungu alitaka kuongea
kwa wengine ambayo yanamfanya Mungu afanye mabadiliko katika maisha yao.
Sala: Bwana, nipe maneno yako ya kuongea. Nisaidie mimi
nikurudie wewe ndani ya moyo wangu kwa ujasiri ili uweze kuwa chanzo cha ukweli
na uzuri. Ninaomba ukweli huo utoke ndani mwangu kila siku. Ninaomba wote
wakuone wewe kwa njia ya maisha yangu. Yesu nakuamini wewe. Amina.
Copyright ©2013-2026 ©FurKat, Furaha ya
Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com

No comments:
Post a Comment