
“KUFUFUKA NA KRISTO”
Tafakari ya Pasaka
Alhamisi, Mei 1, 2025.
Juma la 2 la Pasaka
Kumbukumbu ya Mt. Yosefu Mfanyakazi
Mwa 1:26-2:3; au Mdo 5:27-33
Zab 90:2-4, 12-14, 16 (K. 17);
Yn 3:31-36 au Mt 13:54-58.
MT. YOSEFU MFANO WA WAFANYA KAZI
Injili ya leo inaongelea kuhusu lile
kundi la watu wanaomtafuta Yesu, siku baada ya kuongeza ile mikate. Kumtafuta
huku haikuwa kwasababu ya upendo kwake, bali kufaidika kutoka kwake. Yesu,
anawaambia wazi kwamba wanamtafuta kwasababu walikula mikate, Yesu anawaeleza
wawe na lengo lingine la kumtafuta. Sababu iwe ni kwasababu anataka kuwapa
chakula cha kiroho.
“Je, unamtafuta Yesu kwasababu njema?”
pengine mara nyingi tunamtafuta Yesu kwasababu ya faida fulani, pengine ili
kupata gari, nyumba, mchumba, uponyaji wa ugonjwa. Yesu anatuonya tuangalie
tusimtafute kwasababu ya vitu vinavyo haribika tu, bali tutafute uzima wa
milele.
Kanisa leo lina adhimisha kumbukumbu ya Mt.
Yosefu Mfanyakazi. Mungu alimwamini na kumpa jukumu la kumtunza Mama wa Mungu
na Mwana wa Mungu, na kuwa mlinzi wa nyumba ya Mungu. Hakuna mtu mwingine
yeyote aliyekuwa na nafasi hii pekee. Kupenda kwake kazi ilionesha unyenyekevu
wake, aliishi kwa kadiri ya matakwa ya Mungu. Alikuwa mtu mwenye haki. Kilicho
mfanya akubalike machoni pa Mungu ilikuwa kwasababu ya Imani yake na utii wake.
Kujitoa kwake kulionesha unyenyekevu na kumtegemea Mungu. Na hata baada ya kupata
upendeleo kutoka kwa Mungu, hakuacha kufanya kazi.
Katika hali hii tunaweza kusema kwamba yeye
ni somo wa wale wote wanaofanya kazi, kazi ambayo ni kuonesha unyenyekevu na
tegemeo letu kwa Mungu. Leo tunawakumbuka watu wote duniani wanao fanya kazi kwa
manufaa ya uzuri wa wanadamu wote. Tuwaombee kazi zao zisiharibu mpango wa
Mungu kwa mwanadamu bali zilinde utu na uhai wa kila mwanadamu kama Mt. Yosefu
alivyo linda uhai wa Yesu dhini ya Herode.
Sala: Asante, Mt. Yosefu kwa kumfundisha Yesu
kufanya kazi yako. Tunakushukuru kwa kuzipa kazi za mikono thamani na
utakatifu. Tunaomba tuweze kuzipa heshima kazi na kuwa tayari kwa ajili ya
wengine kama wewe. Mt. Yosefu, mlinzi wa nyumba ya Mungu. Utuombee.
No comments:
Post a Comment