Everyday Saint / Maisha ya Watakatifu

NOVENA YA HURUMA YA MUNGU SIKU YA TATU: DOMINIKA YA PASAKA




NOVENA YA HURUMA YA MUNGU
SIKU YA TATU: DOMINIKA YA PASAKA


NAMNA YA KUFANYA NOVENA KWA HURUMA YA MUNGU

Sala ya kutubu:
Mungu wangu, ninatubu sana dhambi zangu, kwani ndiwe mwema, ndiwe mwenye kupendeza, wachukizwa na dhambi, basi sitaki kukosa tena, nitafanya kitubio, naomba neema yako nipate kurudi kwako, Amina.

Nia ya sala za leo:
SIKU YA TATU

Maneno ya Bwana Yesu: “Leo niletee roho za watu wenye uaminifu na uchaji wa Mungu, na uwazamishe katika Bahari Kuu ya Huruma yangu. Roho za watu hawa ndizo zilizonifariji katika njia ya Msalaba. Wao ndio waliokuwa tone lile la faraja nilipokuwa katikati ya bahari ya uchungu na mateso.”

Tuwaombee watu wote waaminifu na wenye ibada ambao walimtuliza Yesu katika mateso yake.

W. Ee Yesu mpole na mwenye huruma sana, Wewe huchota neema kwa wingi kutoka katika hazina Yako, na kuzigawa kwa ukarimu kwa kila mmoja wetu na kwa watu wote. Tunakuomba utupokee katika makao ya Moyo wako mpole na wenye huruma nyingi, na usituache tutoroke humo kamwe. Tunakuomba neema hii, kwa ajili ya mapendo ya ajabu, yawakayo moyoni mwako kwa Baba yako wa mbinguni. Amina.

Baba yetu ……. Salamu Maria …… Atukuzwe ……

W. Baba wa Milele, elekeza macho yako yenye huruma, kwa watu wote walio waaminifu, kama vile kwenye hazina na urithi wa Mwanao. Kwa ajili ya mateso yake ya kuhuzunisha, uwajalie Baraka zako, na ulinzi wako daima. Kwa njia hii, waweze kuimarika katika upendo, na wala wasije wakapoteza hazina bora ya Imani Tashi Takatifu, bali, pamoja na majeshi yote ya malaika na watakatifu, waweze kuisifu na kuitukuza huruma yako isiyo na mwisho, kwa milele yote. Amina.


Rozari  ya Huruma ya Mungu
(Tumia chembe za rozari ya kawaida)
Baba yetu …       Salamu Maria …. x3            Nasadiki kwa Mungu Baba Mwenyezi …….

Kwenye chembe kubwa
Baba wa Milele, ninakutolea Mwili na Damu, Roho na Umungu, wa Mwanao Mpenzi sana, Bwana wetu Yesu Kristu, kwa ajili ya malipizi ya dhambi zetu, na dhambi za dunia nzima.

kwenye chembe ndogo
Mwanzishaji: Kwa ajili ya mateso makali ya Bwana wetu Yesu Kristo,
Wote huitika: Utuhurumie sisi na dunia nzima.

Mwisho wa Rozari sali mara tatu sala ifuatayo:
Mungu Mtakatifu, Mtakatifu mwenye Enzi, Mtakatifu unayeishi milele, Utuhurumie sisi na dunia nzima.


Litania ya Huruma ya Mungu



No comments:

Post a Comment