Everyday Saint / Maisha ya Watakatifu

NOVENA YA HURUMA YA MUNGU SIKU YA NNE: JUMATATU BAADA YA PASAKA




NOVENA YA HURUMA YA MUNGU
SIKU YA NNE: JUMATATU BAADA YA PASAKA


NAMNA YA KUFANYA NOVENA KWA HURUMA YA MUNGU

Sala ya kutubu:
Mungu wangu, ninatubu sana dhambi zangu, kwani ndiwe mwema, ndiwe mwenye kupendeza, wachukizwa na dhambi, basi sitaki kukosa tena, nitafanya kitubio, naomba neema yako nipate kurudi kwako, Amina.

Nia ya sala za leo:
SIKU YA NNE

Maneno ya Bwana Yesu: “Leo niletee wale wote wasioniamini na wale wasionijua bado. Wao pia niliwafikiria wakati wa mateso yangu makali, na juhudi watakayokuwa nayo baadaye ilinituliza Moyo wangu. Uwaingize katika Bahari Kuu ya Huruma Yangu.”

Tuwaombee watu wote wasiomwamini Kristu, pamoja na wale wasiomjua bado.

W. Ee Yesu mwema, Wewe ni Mwanga wa dunia nzima, uzipokee katika makao ya Moyo wako wenye huruma sana, roho za wale wote wasiokuamini na wale wasiokujua bado. Achia mionzi ya neema yako iwaangazie, ili nao pia pamoja nasi sote. Waweze kuitukuza huruma yako ya ajabu, na usiwaache wakatoroka makao hayo, ambayo ni Moyo wako uliojaa huruma. Amina.

Baba yetu ……… Salamu Maria ……. Atukuzwe ………

W. Baba wa Milele, elekeza macho yako yenye huruma, kwa roho za watu wale wasiomwamini Mwanao, na za wale ambao hawajakujua Wewe bado, ambao tumewaingiza ndani ya Moyo wa Yesu uliojaa huruma tele. Uwavute kwenye mwanga wa Injili, watu hawa hawajui Ukuu wa furaha iliyopo katika kukupenda Wewe. Uwajalie nao pia waweze kuitukuza hisani ya huruma yako, kwa miaka isiyo na mwisho. Amina.

Rozari  ya Huruma ya Mungu
(Tumia chembe za rozari ya kawaida)
Baba yetu …       Salamu Maria …. x3            Nasadiki kwa Mungu Baba Mwenyezi …….

Kwenye chembe kubwa
Baba wa Milele, ninakutolea Mwili na Damu, Roho na Umungu, wa Mwanao Mpenzi sana, Bwana wetu Yesu Kristu, kwa ajili ya malipizi ya dhambi zetu, na dhambi za dunia nzima.

kwenye chembe ndogo
Mwanzishaji: Kwa ajili ya mateso makali ya Bwana wetu Yesu Kristo,
Wote huitika: Utuhurumie sisi na dunia nzima.

Mwisho wa Rozari sali mara tatu sala ifuatayo:
Mungu Mtakatifu, Mtakatifu mwenye Enzi, Mtakatifu unayeishi milele, Utuhurumie sisi na dunia nzima.


Litania ya Huruma ya Mungu

No comments:

Post a Comment