NOVENA YA HURUMA YA MUNGU
SIKU YA PILI: JUMAMOSI KUU
NAMNA YA KUFANYA NOVENA KWA
HURUMA YA MUNGU
Sala ya kutubu:
Mungu wangu, ninatubu sana dhambi
zangu, kwani ndiwe mwema, ndiwe mwenye kupendeza, wachukizwa na dhambi, basi
sitaki kukosa tena, nitafanya kitubio, naomba neema yako nipate kurudi kwako,
Amina.
Nia ya sala za leo:
SIKU YA PILI
Maneno ya Mwokozi: “Leo niletee
mapadri wote na watawa. Uwazamishe katika kilindi cha huruma yangu isiyo na
mwisho. Ni wao hasa walionipa nguvu ya kuweza kuyavumilia mateso yangu makali
mno. Kwa njia yao, kama vile mifereji, huruma yangu humiminika na kuwatiririkia
wote. Tuwaombee watawa wote wanawake ili wadumu kiaminifu katika utumishi wao
na wakfu wa maisha yao kwa Yesu Kristu Bwanaharusi wao.”
W. Ee Yesu mwenye huruma tele, kwako hutoka mema yote. Uwazidishie neema yako
watawa wanawake waliojitolea na kuwekwa wakfu katika utumishi wako, ili
watekeleze utumishi wao kwa huruma na kwa jinsi inayofaa, na kwamba wale
wanaowaona na kuzishuhudia kazi zao bora, waweze kumtukuza Baba wa Huruma aliye
mbinguni. Amina.
Baba yetu ……. Salamu Maria …… Atukuzwe
……
Tuwaombee mapadri na watawa wote ambao ni vyombo vya huruma
ya Mungu.
W. Baba wa
Milele, elekeza macho yako yenye huruma, juu ya jeshi teule la wafanyakazi
shambani mwako. Uzitazame kwa wema roho zao mapadre na watawa wote. Uwajalie
wingi wa Baraka zako. Kwa njia ya upendo wa Moyo wa Mwanao, humo ambamo
wameingizwa, uwape nguvu na mwanga, ili waweze kuwaongoza wengine katika njia
ya wokovu, na kwa sauti moja, waihimidi huruma yako kwa nyimbo za sifa bila
mwisho. Amina.
Rozari ya Huruma ya Mungu
(Tumia chembe za rozari ya kawaida)
Baba yetu
… Salamu Maria ….
x3 Nasadiki
kwa Mungu Baba Mwenyezi …….
Kwenye chembe kubwa
Baba wa Milele, ninakutolea
Mwili na Damu, Roho na Umungu, wa Mwanao Mpenzi sana, Bwana wetu Yesu Kristu,
kwa ajili ya malipizi ya dhambi zetu, na dhambi za dunia nzima.
kwenye chembe ndogo
Mwanzishaji: Kwa ajili ya mateso
makali ya Bwana wetu Yesu Kristo,
Wote huitika: Utuhurumie sisi na dunia nzima.
Mwisho wa Rozari sali mara
tatu sala ifuatayo:
Mungu Mtakatifu, Mtakatifu
mwenye Enzi, Mtakatifu unayeishi milele, Utuhurumie sisi na dunia nzima.
Litania ya Huruma ya Mungu
No comments:
Post a Comment