“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya kila siku
Jumanne, Septemba 5, 2023,
Juma la 22 la Mwaka wa Kanisa
Kumbukumbu ya Mt. Teresia wa Kolkota.
1 Thes 5: 1-6, 9-11;
Zab 27: 1, 4, 13-14;
Lk 4: 31-37
WATOTO WA MWANGA
Yesu ambaye aliweza kuonesha “mvuto mkubwa wa ndani sana” wakati
anafundisha. Na walifananisha na mamlaka aliyo ongelea. Yesu hakuwa kuhani wa
kipindi hicho, wala Mfarisayo au mwalimu wa sheria. Hawa ndio watu waliokuwa na
mamlaka ya kufundisha na kufafanua neno la Mungu. Watu waliuliza “ni kitu ghani
kilichopo katika mafundisho yake”, neno lake lilikuwa na mvuto na msukumo
mkubwa kwasababu ya uhusiano wake na Baba yake. Maneno ya Yesu yalibeba mamlaka
na msukumo mkubwa.
Mamlaka hayo hayo tumepewa sisi wote, kila Mkristo. Tunaitwa kutoa ushuhuda
na kuhubiri. Furaha ya Injili tunayo hubiri au kuongea juu yake inabeba nguvu
zaidi tunapokuwa na msukumu wa Yesu katika maisha yetu. Maneno yetu yanagusa
mioyo ya watu yanapo toka katika chemchem hii ya furaha. Paulo akitumia mfano
wa kulala na kuamka, anatuambia kwamba tutambue kwamba sisi ni watoto wa
Mwanga, tunaojiandaa kwa ajili ya utukufu wa mbinguni, hivyo tunapaswa kuishi
kama mwanga ulivyo. Sisi tunaitwa kutoa maisha ya ushuhuda, hatupaswi kuwa
wakristo wa uvuguvugu, wavivu na walio lala, bali wachangamfu, wenye uhai na
furaha, tuliojazwa na neno la upendo wa Kristo na Injili yake. Moto huu ndio
ule moto alio udhihirisha Yesu wakati akihubiri neno, na kutoa pepo. Hili ndilo
Kristo anapenda na sisi tufanye pia.
Leo tunasherekea , kumbukumbu ya Mt. Teresa wa Kolkota. Huyu mtakatifu
alijazwa na upendo na msukumo wa Kristo. Aliongea kwa matendo yake, kuwalisha
wenye njaa, kuwapa maji wenye kiu, akiwahudumia wagonjwa na wanao teseka, na
kujali utu wao waliokuwa katika kufa. Alikuwa ni shuhuda wa upendo, katika
jamii ambayo upendo ulikuwa umetelekezwa. Na akaanza kuleta mwanga katika giza
kwa wale waliokuwa wamepotea, kunyanyaswa na kutengwa. Tujifunze leo katika
liturjia ya leo jinsi ya kuwa watu wa mwanga.
Sala: Asante Bwana Yesu, kwa upendo wako na huruma yako. Umetubariki sisi
na kutushirikisha katika mamlaka yako na msukumo wako, tuwe mwanga katika
ulimwengu uliojazwa giza. Nipe nguvu mimi niweze kuwa karibu nawe na niwe mtoto
wa mwanga. Yesu, nakuamini wewe. Amina.
Amina
ReplyDelete