MASOMO YA MISA, JUMANNE , SEPTEMBA 5, 2023
JUMA LA 22 LA MWAKA
Kumbukumbu ya Mtakatifu Teresia wa Kolkota
Kumbukumbu ya Mtakatifu Teresia wa Kolkota
________
SOMO 1
1The. 5:1-6, 9-1
Ndugu, kwa habari ya nyakati na majira, hamna
haja niwaandikie. Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja
kama vile mwivi ajavyo usiku. Wakati wasemapo, Kuna Amani na salama, ndipo
uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala
hakika hawataokolewa.
Bali ninyi, ndugu, hammo gizani, hata siku ile
iwapate kama mwivi. Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa nuru, na wana wa
mchana; sisi si wa usiku, wala wa giza. Basi tusilale usingizi kama wengine,
bali tukeshe, na kuwa na kiasi. Kwa kuwa Mungu hakutuweka kwa hasira yake, bali
tupate wokovu, kwa Bwana wetu Yesu Kristo; ambaye alikufa kwa ajili yetu, ili
tuishi pamoja naye, kwamba twakesha au kwamba twalala. Basi, farijianeni na
kujengana kila mtu na mwenzake, vile vile kama mnavyofanya.
Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.
________
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 27:1,4, 13-14 (K) 13
(K) Naamini
ya kuwa nitauona wema wa Bwana katika nchi ya walio hai.
Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu,
Nimwogope nani?
Bwana ni ngome ya uzima wangu,
Nimhofu nani? (K)
Neno moja nimelitaka kwa Bwana,
Nalo ndilo nitakalolitafuta,
Nikae nyumbani mwa Bwana,
Siku zote za maisha yangu.
Niutazame uzuri wa Bwana,
Na kutafakari hekaluni mwake. (K)
Naamini ya kuwa nitauona wema wa Bwana,
Katika nchi ya walio hai.
Umngoje Bwana, uwe hodari,
Upige moyo konde, naam, umngoje Bwana. (K)
________
________
SHANGILIO
2Tim. 1:10
Aleluya, aleluya,
Mwokozi wetu Yesu Kristu alibatili mauti,
na kuufunua uzima na kutokuharibika kwa Injili.
na kuufunua uzima na kutokuharibika kwa Injili.
Aleluya.
________
INJILI
Lk. 4:31 – 37
Yesu alishuka mpaka Kapernaumu, mji wa Galilaya,
akawa akiwafundisha siku ya sabato; wakashangaa mno kwa mafundisho yake, kwa
kuwa neno lake lilikuwa na uwezo.
Na ndani ya sinagogi mlikuwa na mtu mwenye roho
ya pepo mchafu, akalia kwa sauti kuu, akisema, Acha! Tuna nini nawe, Yesu wa
Nazareti? Umekuja kutuangamiza? Nakujua u nani, Mtakatifu wa Mungu. Yesu
akamkemea, akisema, Fumba kinywa, mtoke. Ndipo yule pepo akamwangusha katikati,
akamtoka asimdhuru neno. Mshangao ukawashika wote, wakasemezana wakisema, Ni
neno gani hili, maana awaamuru pepo wachafu kwa uwezo na nguvu, nao hutoka.
Habari zake zikaenea kila mahali katika nchi ile.
Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
______
Copyright © 2023, "MASOMO YA MISA"
published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania. Readings reproduced by
Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment