“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya kila siku
Jumatatu, Septemba 4, 2023
Juma la 22 la Mwaka
___________________
1 Thes 4: 13-18;
Zab 96:1-5, 11-13;
Lk 4:16-30
___________________
KRISTO ANAONGEA NASI KWA NJIA YA FAMILIA NA MARAFIKI ZETU!
Kwa ujumla tukitazama maisha yetu, inaweza kuwa vigumu kuongelea mambo ya kiroho, Biblia na Yesu na familia zetu, ndugu na marafiki tukilinganisha na kuongea na watu tusio wajua. Inaweza ikawa tena ngumu zaidi kwa sisi wenyewe kushindwa kuona jambo lolote zuri la kiroho tunalo weza kujifunza kutoka kwa wenzetu. Inaweza kuwa tunaogopa kuchekwa au kukataliwa.
Leo Yesu anasomo sehemu ya maandiko katika chuo cha nabii Isaya, hekaluni, mbele ya ndugu zake. Yesu anaendelea kusema “hakuna nabii anaye kubalika nyumbani kwake mwenyewe”. Jamaa zake walimsikiliza na walivutwa sana, lakini wakaanza kuhitimiza mara moja kwamba huyu hana kitu, si mwana wa seremala? Mwishoni wanashikwa na hasira na wanamtoa Yesu nje wakitaka kumua.
Kama Mwana wa Mungu alipata wakati mgumu wa kukubalika katika jamaa yake mwenyewe, itakuwa vigumu pia kushirikishana Injili na wale walio karibu yetu. Lakini kilicho cha muhimu inategemea tuna fanyaje au hatumuone Kristo katika wale walio karibu yetu? Je, sisi ni mmoja wapo wa wale wasiopenda au kukataa kumuona Kristo katika ndugu zetu wa familia na wa karibu? Je, tunakuwa watu wakuhukumu wale walio karibu yetu?
Ukweli ni kwamba ni rahisi kwetu sisi kuona makosa ya wale walio karibu yetu kuliko kuona fadhila zao. Ni rahisi zaidi kuona dhambi zao kuliko kuona uwepo wa Kristo katika maisha yao. Lakini sio kazi yetu kunyoosha kidole juu ya dhambi zao. Ni jukumu letu kumuona Mungu ndani yao. Kila mtu aliye karibu yetu bila kuwa na shaka, ana uzuri ndani yake. Watakuwa na hali ya kumtafakari Mungu kama sisi tupo tayari kuliona kwao zaidi. Kazi yetu haipaswi kuliona hilo tu bali kulitafuta ndani yao. Na tunapo kuwa karibu zaidi kati yao ndivyo tunavyopaswa kuchunguza zaidi uwepo wa Mungu ndani ya maisha yao.
Tafakari leo, kama upo tayarii kutaka kuona unabii wa sauti ya Kristo ulio ndani ya watu walio karibu yako. Je, upo tayari kuona, kumkubali na kumpenda yeye ndani yao?
Sala: Bwana, ninakuomba nikuone wewe kwa wale wote waliokaribu yangu kila siku. Ninakuomba nikutafute wewe zaidi katika maisha yao. Na ninapo kupata wewe ndani yao, nikupende wewe ndani yao. Yesu, nakuamini wewe. Amina

Copyright ©2013-2023 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment