MASOMO YA MISA, JUNI 13, 2023
JUMANNE, JUMA LA 10 LA MWAKA
KUMBUKUMBU YA MTAKATIFU ANTONI WA PADUA
SOMO 1
2Kor. 1:18 – 22
Kama Mungu alivyo mwaminifu, neno letu kwenu si
Nidyo na siyo. Maana Mwana wa Mungu, Kristo Yesu, aliyehubiriwa katikati yenu
na sisi, mimi na Silwano na Timotheo, hakuwa Ndiyo na siyo; bali katika yeye ni
Ndiyo. Maana ahadi zote za Mungu zilizopo katika yeye ni Ndiyo; tena kwa hiyo
katika yeye ni Amin; Mungu apate kutukuzwa kwa sisi. Basi Yeye atufanyaye imara
pamoja nanyi katika Krito, na kututia mafuta, ni Mungu, naye ndiye aliyetutia
muhuri akatupa arabuni ya Roho mioyoni mwetu.
Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 119:129 – 133, 135 (K) 135
(K) Umwangazie mtumishi wako uso wako.
Shuhuda zako ni za ajabu,
Ndiyo maana roho yangu imezishika.
Kufafanusha maneno yako kwatia nuru,
Na kumfahamisha mjinga. (K)
Nalifunua kinywa changu nikatweta,
Maana naliyatamani maagizo yako.
Unigeukie, unirehemu mimi,
Kama iwahusuvyo walipendao jina lako. (K)
Uzielekeze hatua zangu kwa neno lako,
Uovu usije ukanimiliki.
Umwangazie mtumishi wako uso wako,
Na kunifundisha amri zako. (K)
SHANGILIO
Zab. 19:18
Aleluya, aleluya.
Amri ya Bwana ni safi, huyatia macho nuru.
Aleluya.
INJILI
Mt 5: 13-16
Yesu aliwaambia wanafunzi wake: Ninyi ni chumvi
ya dunia; lakini chumvi ikiwa imeharibika itatiwa nini hata ikolee? Haifai tena
kabisa, ila kutupwa nje na kukanyagwa na watu. Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji
hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima. Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini
ya pishi, bali juu ya kiango; nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani. Vivyo
hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema,
wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.
Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
Copyright © 1993 T.M.P. Book Department, Tabora - Tanzania: see MASOMO YA
MISA. Scripture readings from ‘Biblia Takatifu’are published and copyright ©
1975, 1993 by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania.© Bible Society of
Kenya, © Bible Society of Tanzania.These readings are a reproduction by Furaha
ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment