“KUFUFUKA NA KRISTO”
Tafakari ya Pasaka
Jumamosi, Mei, 13, 2023.
Juma la 5 la Pasaka
Mdo 16: 1-10;
Zab 100: 1-3,5 (R. 1);
Yn 15: 18-21.
KUKUTANA NA MATESO
Mkristo kwa Sakramenti ya Ubatizo ni mmisionari. Anaitwa kushirikisha
Habari Njema kwa kila mtu . katika ubatizo, Mkristo hufufuka kutoka katika hofu
ya kifo, na kwenda kwenye utukufu wa uzima wa milele. Sisi sio watu tuliofungwa
na dunia bali watu tuliofungwa na Mbinguni. Na hii safari ya kwenda mbinguni
sio rahisi, kwasababu thamani na hali ya maisha ya Kikristo ni tofauti na hali
ya kawaida ya kufikiri.
Ni rahisi kufikiri kwamba kadiri tunavyokuwa karibu na Yesu ni kadiri hiyo
hiyo tutakavyo pendwa na kueleweka na Ulimwengu. Tunadhani kwamba kila mtu
atapendezwa na kuvutwa na utakatifu wetu na kuwa watu wazuri kwetu. Lakini
sivyo. Tukiangalia maisha ya Yesu, tunatambua kuwa haikuwa hivyo. Alikuwa wazi
ni mkamilifu kwa kila kitu. Lakini, walimtenda vibaya na kumsulubisha.
Alishikwa na kupigwa na kutukanwa na kuhukumumiwa kifo.
Kama tungekuwa pale, tungeweza kushangazwa sana, na kuchanganyikiwa.
Tunaweza kufikiri kwamba Yesu alikosea na hivyo kupoteza matumani kwake. Lakini
mpango wake ulikuwa mkamilifu kwa kila njia na mpango wake ulikuwa katikati na
kumfanya yeye kuvumilia dhuluma za uongo na kuteswa. Na kwa uhuru kukubali
kushutumiwa, aliikomboa dunia.
Ukristo ni dini inayo onewa kuliko zote duniani. Asimilia kumi ya wakristo
ulimwenguni wananyanyaswa na kuonewa kwasababu tu ya imani yao. Kunyanyaswa na
kuonewa kunaleta hofu na uchungu. Lakini sio kitu ambacho tunapaswa kukikimbia.
Hatupaswi kupoteza matumaini yanavyotokea haya. Kwanini? Kwasababu manyanyaso
ni ishara wazi tunafuata njia sahihi ya Yesu. Tumeungana na Yesu zaidi katika
njia ya kuonewa na kudhulimiwa kuliko hata tunavyofikiri. Ufunguo ni kutambua
kwamba Mungu atatumia madhulumu yote kuwa furaha yetu kama tutamruhusu. Na
tutamrushu ayatumie kwa kuleta mema kama tutajikabidhi kwake kwa uhuru kabisa.
Majibu yetu yanapaswa kuwa “furahi na kushangilia” kwani tumekuwa sahihi katika
kufuata njia ya Bwana wetu, Mwana wa Mungu.
Leo tutazame katika hali yeyote ya kuonewa na kudhulumiwa au kukosewa haki
tunayo ipata kwasababu ya Imani yetu na kushika Injili. Tuwaombee pia Wakristo
wanaodhulumiwa huko Syria, Misri, China, Pakistani, India nk.
Sala: Bwana, nina kabidhi kwako yale yote yanayo niangusha chini. Ninatoa
sadaka yote ninayo pokea kwa kuwa mtumishi na mfuasi wako. Ninaomba nisikuige
wewe tu katika mateso yako, bali kutii mapenzi yako daima. Yesu, nakuamini
wewe. Amina
No comments:
Post a Comment