MASOMO YA MISA, MEI 13, 2023
JUMAMOSI, JUMA LA 5 LA PASAKA
SOMO 1
Mdo 16:1-10
Siku zile, Paulo alifika Derbe na Listra na hapo
palikuwa na mwanafunzi mmoja jina lake Timotheo, mwana wa mwanamke Myahudi
aliyeamini; lakini babaye alikuwa Myunani. Mtu huyo alishuhudiwa vema na ndugu
waliokaa Listra na Ikonio. Paulo akamtaka huyo afuatane naye, akamtwaa
akamtahiri kwa ajili ya Wayahudi waliokuwako pande zile; kwa maana wote walijua
ya kuwa babaye ni Myunani. Basi walipokuwa wakipita kati ya miji ile, wakawapa
zile amri zilizoamriwa na mitume na wazee walioko Yerusalemu, ili wazishike. Makanisa
yakatiwa nguvu katika ile Imani, hesabu yao ikaongezeka kila siku.
Wakapita katika nchi ya Frigia na Galatia,
wakikatazwa na Roho Mtakatifu, wasilihubiri lile neno katika Asia. Walipofika
kukabili Misia, wakajaribu kwenda Bithinia, lakini Roho wa Yesu hakuwapa
ruhusa, wakapita Misia wakatelemka Troa. Paulo akatokewa na maono usiku;
alimwona mtu wa Makedonia amesimama, akimsihi, na kumwambia, Vuka, uje
Makedonia utusaidie. Basi alipo- kwisha kuyaona vale maono, mara tukataka
kutoka kwenda Makedonia. kwa kuwa tuliena hakika ya kwamba Mungu ametuita
tuwahubiri Habari Njema.
Neno la Bwana... Tumshukuru Mungu.
WIMBO WA KATI KATI
Zab. 100 :1-3, 5 (K) I
(K) Mfanyieni Bwana shangwe, dunia yote. au:
Aleluya.
Mfanyieni Bwana shangwe, dunia yole.
Mtumikieni Bwana kwa furaha.
Njoni mbelc zake kwa kuimba; (K)
Jueni kwamba Bwana ndiye Mungu;
Ndiye aliyetuumba na sisi tu watu wake:
Tu watu wake, na kondoo wa malisho yake. (K)
Kwa kuwa Bwana ndiye mwema;
Rehema zake ni za milele;
Na uaminifu wake vizazi na vizazi. (K)
SHANGILIO
Yn. 20-29
Aleluya, aleluya,
Wewe Toma, umesadiki kwa kuwa umeniona, wa heri
wale wasioona wakasadiki.
Aleluya,
INJILI
Yn 15 : 18-21
Siku ile, Yesu aliwaambia wanafunzi wake: Iwapo
ulimwengu ukiwachukia, mwajua ya kuwa umenichukia mimi kabla ya kuwachukia
ninyi. Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungewapenda walio wake; lakini kwa
kuwa ninyi si wa ulimwengu, bali mimi naliwachagua katika ulimwengu, kwa sababu
hiyo ulimwengu huwachukia. Likumbukeni lile neno nililowaambia, Mtumwa si
mkubwa kuliko bwana wake. Ikiwa waliniudhi mimi, watawaudhi ninyi; ikiwa
walilishika neno langu watalishika na lenu. Lakini haya yote watawatenda kwa
ajili ya jina langu, kwa kuwa hawamjui yeye aliyenipeleka.
Neno la Bwana... Sifa kwako Ee Kristo.
Copyright © 1993 T.M.P. Book Department, Tabora - Tanzania: see MASOMO YA
MISA. Scripture readings from ‘Biblia Takatifu’are published and copyright ©
1975, 1993 by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania.© Bible Society of
Kenya, © Bible Society of Tanzania.These readings are a reproduction by Furaha
ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment