“KUFUFUKA NA KRISTO”
Tafakari ya Pasaka
Jumamosi, Mei 20, 2023.
Juma la 6 la Pasaka
Mdo 18: 23-28
Zab 47: 2-3, 8-10 (R. 8);
Yn 16: 23-28.
KUELEWA NENO LA MUNGU!
Katika somo la kwanza kutoka katika kitabu cha matendo ya Mitume, kina
muongelea mtu mmoja ambaye anaitwa Apollo ambaye ni mfano kwa wakristo wote.
Alifahamu maandiko na alikuwa na ujasiri wa kuhubiri habari njema. Alifanya
watu wengi wabadilishe maisha yao na kuongoka, kwa kutangaza Neno la Mungu. Sio
wote walio na uweze wa kufafanua Neno la Mungu. Tunahitaji msaada wa Mungu na
uongozi wa Roho Mtakatifu. Ufufuko wa Bwana wetu Yesu Kristo umefungua milango
ya neema. Tunaweza kuomba kwa Mungu kwa jina la Kristo na nguvu ya Roho
Mtakatifu.
Maandiko Matakatifu, na hasa mafundisho ya Kristo yapo katika lugha ambayo
imefunikwa kiasi kikubwa, ambayo sio wote waweza kuelewa. Kwahiyo kwanini Yesu
anaongea katika lugha ambayo imefunikwa au kufichwa na asiongee kwa wazi wazi
moja kwa moja? Jibu linahusika na sisi ukosefu wetu wa kutokuwa wazi katika
ukweli. Kama tunakuwa wazi katika ukweli, na kuwa tayari kukumbatia ukweli bila
kujali ni namna ghani, Yesu angeongea nasi na sisi kuitika mara moja. Lakini
sivyo ilivyo. Ufunguo wa kuelewa haya ni kuelewa na kutambua elimu ya mapenzi
ya Mungu na utayari wa kutimiza mapenzi hayo. Mara nyingi sisi tunataka Yesu
atuambie mapenzi yake, tufikirie juu yake, na kuangalia, alafu sisi tunakuja na
majibu yetu wenyewe. Lakini kama tunataka Yesu aongee nasi wazi wazi, tunapaswa
kusema ndio kwa Yesu hata bila kutambua anataka tufanye nini. Utayari wa
kukubali mapenzi yake ni mwanzo wa kuelewa mapenzi yake.
Mfano kamili wa hili ni Mama yetu Bikira Maria. Kbala ya Malaika kuja kwake
yeye alikuwa akiyashika mapenzi ya Mungu. na Malaika alipofika na kumwelezea
nini kitacho tokea, yeye aliuliza uelewa zaidi. Na kweli alipata kuelewa zaidi
kwa kupata jibu kwa swali lake. Lakini sababu moja ya malaika, kama mjumbe wa
Mungu, aliongea wazi wazi kwasababu alishafahamu wazi moyo wa Maria kuwa
unamtegemea Mungu bila kujali kutatokea nini.
Je, unataka Mungu aongee nawe katika hali ya uwazi? Je, unataka kuelewa
Neno la Mungu? kama ndivyo, sema ndio kwa kile ambacho Mungu anapenda wewe
utende daima. Kwa kujenga hali hii ya kusema ndio kwa mapenzi ya Mungu,
itamfanya Mungu kukufungulia mlango mara moja kuelewa yale yote anayotaka
uyatende katika kutimiza mapenzi yake.
Sala: Bwana, ninachagua mapenzi yako leo na daima. Sichagui kitu kingine ni
mapenzi yako tu. Ninavyosema ndio kwako, nisaidie niweze kukuwa katika hali ya
uwazi wako unaopenda. Yesu, ninakuamini wewe. Amina
No comments:
Post a Comment