“KUFUFUKA NA KRISTO”
Tafakari ya Pasaka
Ijumaa, Mei, 19, 2023,
Juma la 6 la Pasaka
Mdo 18: 9-18;
Zab 47: 2-7 (R. 8);
Yn 16: 20-23.
FURAHA NA TUMAINI LA UFUFUKO!
Kila tukio katika maisha yetu linaleta matokeo fulani katika maisha yetu.
Wakati matokeo yakiwa mazuri tunakuwa na furaha. Na wakati tukiwa tunazamia
mazuri yatokee hilo tunaita kuwa tumaini. Kama matokeo ni mabaya tunakuwa na
huzuni na tunakuwa na hofu na mashaka. Hali hizi zinabadilika kadiri ya hisia
zetu, na hayabakii kuwa yale yale. Injili inayaweka yote haya katika mfano wa
kuzaliwa kwa mtoto. Kunakuwepo na maumivu, hofu lakini furaha huja baadae.
Tunapaswa kuwenda zaidi ya haya tunayo yaona ulimwenguni ili tuweze kwenda
kufuhia furaha ya ufalme wa Mungu. Kama Yesu alivyokufa juu ya vitu vyote ili
afufuke katika utukufu wa Mungu, hivyo hivyo nasi tunapaswa tufe juu ya mambo
yanayoleta furaha ya muda na kwa kufanya hivi lazima tuhizi uchungu wa kuacha baadhi
ya mambo ili tuweze kufufuka ndani Yake. Maisha yanakuwa kwa kuyatoa, lakini
yanaharibika kwa kujitenga na kujifariji binafsi.
Je, mateso yana maana kwamba upo mbali na Mungu? Au hauna neema ya Mungu?
Ina maana kwamba Mungu amekuacha? Au ina maana kwamba unafanya kitu kibaya?
Hakika sio hivyo, tunachopaswa kufanya nikuangalia maisha ya Yesu na tutatambua
kwamba hili halipo hivyo. Alikuwa katika hali ya misuko suko na kupingwa na
viongozi kila wakati lakini alijikita zaidi katika utume wa Baba yake. Alikuwa
akisali kwa siku arobaini jangwani. Katika utume wake alikutana na vipingamizi
vingi sana. Alitukanwa na kupingwa, kutokueleweka, kutemewa mate, na zaidi hata
mpaka alivyokufa msalabani.
Mama yetu Bikira Maria alipatwa na “uchungu kama upanga” ukampenya moyo
wake. Alikuwa na upendo kamili kwa mtoto wake. Aliwaona wengi waliokuwa
wakimpenda mwanae na wale wasiompenda mwanae. Aliwaona wale waliokuwa
wakimsulubisha na kumbebesha msalaba.
Lakini fikiria juu ya maisha yao. Wanafurahi sasa Mbinguni kama watakatifu,
na Mama yetu kama Malkia wa mbinguni na watakatifu wote, na Yesu kama Mfalme wa
Mbingu na Nchi. Wanaishi katika utukufu milele. Huzuni zao zimebadilika na kuwa
furaha kamili. Kama unafikiri umetendewa vibaya au wamekuonea, furahi upo
salama. Tambua kuwa unapo bakia mwaminifu na kutembea katika njia ya uaminifu
ya Mungu aliokuwekea, mwisho ni kwamba utafurahia! Shikilia katika tumaini hilo
na elekeza macho yako katika njia ya Mungu. Hakika utafanikiwa.
Sala: Bwana, ninakabidhi mizigo yangu yote na uchungu wote kwako.
Ninaunganisha na msalaba wako nikitumaini kuwa utakuwa nami katika yote katika
njia yangu ya maisha. Ninaomba niweke moyo wangu katika lengo langu nikiwa na
furaha katika upendo wako kamili. Yesu, nakuamini wewe. Amina
Copyright ©2013-2023 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki:
see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment