“KUFUFUKA NA KRISTO”
Tafakari ya Pasaka
Alhamisi, Aprili 13, 2023
Oktava ya Pasaka
Mdo 3:11-26
Zab 8:2,5-9
Lk 24:35-48
UFUFUKO: KUONDOA HOFU NA KUKUMBATIA FURAHA!
Wakati Wanafunzi wawili wakiwa wanashirikisha habari juu ya tukio la Emaus,
Yesu alitokea kati yao, walishtuka na kuogopa. Yesu katika hali yake ya
Kibinadamu yakuonesha makovu ya madonda yake, kwa kula chakula pamoja nao,
iliwafanya waondoe hofu na kuondoa baadhi ya maswali yaliokuwa yakiwasumbua.
Walimuona Yesu, Bwana wao mpendwa, ambaye amejifunua mwenyewe, ambaye ni
muelewa, ambaye anawasiliana nao, ambaye anasamehe na ambaye anawapa nguvu.
Waliyapokea maneno yake katika hali ya juu sana, na wanafanywa kuelewa habari
yote kuhusu maisha ya Yesu. Watu ambao walifikiri kwamba maisha yao yamefika
mwisho na ulimwengu wao umekwisha, walianza kuona mwanzo wa Ulimwengu mpya.
Hali hii ya Wafuasi inafunua hali ambayo hata sisi tunakutana nayo wakati
Mungu anatuita tuingie katika utukufu na neema yake. Mara nyingi wakati Mungu
anavyotuita karibu naye, wakati anatuita tuweze kuona furaha ua ufufuko,
tunapatwa na mashaka. Tunaweza tukaona ngumu kupokea ukweli wa ufufuko katika
maisha yetu. Hii inaweza kutokea kwasababu mbali mbali. Kukata tamaa inaweza
kuwa sababu yetu kushindwa kukumbatia maisha ya ufufuko. Wafuasi walikatishwa
tamaa kabisa kwa kifo cha Kristo. Na sasa kwamba amefufuka, na alikuwa
amesimama mbele yao, walikuwa na wasi wasi kuachia hali hiyo ya kukata tamaa
iondoke.
Sisi pia, tunaweza tukaacha uzito wa ulimwengu, dhambi zetu au dhambi za
wengine, zitukatishe tamaa. Tunaweza kusikia hasira na kuchukia na tukajikuta
tunashindwa kutoka katika matatizo tunayo kutana nayo. Kuwa na furaha ya
ufufuko maana yake tunarudisha macho yetu na kuangalia ule ukweli ambao Mungu
anapenda sisi tuutazame. Haina maana ya kukatishwa tamaa kwa matatizo mbali
mbali yanayo kuja katika njia zetu. Au kushindwa kumfuata Mungu kwasababu ya
dhambi za wengine. Mungu wetu anatuita tutazame kitu kingine kikubwa zaidi
kuliko matatizo yetu. Anatuita kwenye ushindi wake. Kutazama katika ushindi
wake ni kuwa huru na kuwa na Imani ya hali ya juu katika maisha yetu. Na Imani
hiyo kwa Bwana mfufuka itakuwa na furaha ya ajabu ambayo Mungu anataka tuwe
nayo. Kwa macho yake yakiwa yame elekezwa kwake, yote yale yanayo kushawishi
ukate tamaa yataondoka.
Sala: Bwana, ninataka kukutazama wewe. Ninataka kukuona wewe ukiwa
umefufuka katika wafu na nichukue furaha kubwa katika ukweli huu. Nisaidie,
niweze kuhisi furaha kuu inayotoka kwa kukujua wewe, Bwana wetu mfufuka. Yesu
nakuamini wewe. Amina
No comments:
Post a Comment