NOVENA YA HURUMA YA MUNGU
SIKU YA NANE: IJUMAA BAADA YA
PASAKA
NAMNA YA KUFANYA NOVENA KWA
HURUMA YA MUNGU
Sala ya kutubu:
Mungu wangu, ninatubu sana dhambi
zangu, kwani ndiwe mwema, ndiwe mwenye kupendeza, wachukizwa na dhambi, basi
sitaki kukosa tena, nitafanya kitubio, naomba neema yako nipate kurudi kwako,
Amina.
Nia ya sala za leo:
SIKU YA NANE
Maneno ya Mwokozi wetu: “Leo niletee roho za wale waliofungwa bado toharani, na uwazamishe ndani ya
Bahari Kuu ya Huruma yangu. Humo, mafuriko ya Damu yangu, yazimishe miali ya
motto mkubwa unaowachoma. Roho hizi zote hupendwa sana nami. Wako humo toharani
kwa ajili ya kulipia Haki yangu waliyoikosa hapa duniani. Wewe una uwezo wa
kuwapatia faraja. Chota rehema zote za Kanisa langu na uzitolee kwa ajili yao.
Ungalijua tu ukali wa mateso yao, loo! Ungetolea daima sadaka za kiroho kwa
ajili yao, na kulipa deni zima la Haki ya Mungu”.
Tuwaombee marehemu wa
toharani, wanaoilipia Haki ya Mungu, ili mtiririko wa Huruma wa Damu ya Yesu
uweze kupunguza na kufupisha mateso yao.
W. Ee Yesu mwenye Huruma uliyesema, “Muwe na Huruma kama Baba yenu wa mbinguni
alivyo na Huruma”. Uzitazame kwa Huruma roho zile zinazoteswa toharani, kwa
kulipia deni la Haki ya Mungu waliyoikosea. Mtiririko ule wa Damu na Maji
uliotoka kwa kasi Moyoni mwako, uzimishe miale ya moto mkali wa toharani, ili
huko pia Huruma yako isifiwe na kuadhimishwa. Amina.
Baba yetu ……. Salamu Maria …….
Atukuzwe ………
W. Baba wa Milele, uzitazame kwa wema na huruma, roho zile zinazoteswa
Toharani, wao pia wameingizwa ndani ya Moyo wa Mwanao Mpenzi Yesu, na uchungu
wote ulioelemea Moyo na Roho yake, onyesha Huruma yako kwa roho zilizotiwa
nguvuni na Haki yako. Uwatazame watu hao kwa njia ya Madonda yake Yesu Mwanao
Mpenzi, kwa kuwa tunaamini kabisa kuwa wema na Huruma yako havina mwisho. Amina
Rozari ya Huruma ya
Mungu
(Tumia chembe za rozari ya
kawaida)
Baba yetu
… Salamu Maria ….
x3 Nasadiki
kwa Mungu Baba Mwenyezi …….
Kwenye chembe kubwa
Baba wa Milele, ninakutolea
Mwili na Damu, Roho na Umungu, wa Mwanao Mpenzi sana, Bwana wetu Yesu Kristu,
kwa ajili ya malipizi ya dhambi zetu, na dhambi za dunia nzima.
kwenye chembe ndogo
Mwanzishaji: Kwa ajili ya mateso
makali ya Bwana wetu Yesu Kristo,
Wote huitika: Utuhurumie sisi na dunia nzima.
Mwisho wa Rozari sali mara
tatu sala ifuatayo:
Mungu Mtakatifu, Mtakatifu
mwenye Enzi, Mtakatifu unayeishi milele, Utuhurumie sisi na dunia nzima.
Litania ya Huruma ya Mungu
No comments:
Post a Comment