“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya kila siku
Jumamosi, Januari 21, 2023
Juma la 2 la Mwaka wa Kanisa
Kumbukumbu ya Mt. Agnesi, Bikira na Shahidi
Ebr 9:2-3, 11-14;
Zab 47: 2-3, 6-9;
Mk 3: 20-21
VIPINGAMIZI KATIKA KUMFUATA YESU!
Yesu ni Hekima ya Mungu na ni Mungu. Kila kitu alichofanya na kusema
kilifunua upendo kamili wa Utatu Mtakatifu. Baadhi ya watu walimsikiliza kwa
makini na kwa Imani na utukufu wa mshangao kwa maneno yake na matendo yake.
Waliweza kuona Umungu wake ukingaa na kutambua kweli alikuwa Mwana wa Mungu,
mkombozi wa Ulimwengu. Lakini walikuwepo wengine, hata wengine waliokuwa ndugu
zake, waliodhani “hayupo vizuri kiakili”.
Kama haya yalisemwa kwa Yesu pamoja na ukamilifu wake, yatasemwa pia kwetu
tunaofuata njia zake. Kumfuata Yesu na kutimiza mapenzi yake sio kila mara
itawapendeza ndugu zetu. Yapo mambo mengi tunayoitwa na Injili kufanya na
kusema, ambayo yatapingwa tu na ndugu au jirani zetu. Wakati haya yanatokea,
tusishangae au kuogopa au kutu umiza. Tusipatwe na hasira wala kukata tamaa.
Bali, tunapaswa kujiona wenyewe tukifuata katika njia za Kristo. Tunapaswa
kufikiria pia kuhusu kusingiziwa kwake kwa uongo na kuhukumiwa kwa uongo na
tusikubali tunayosikia kwa wenzetu yatuweke mbali na kufuata mapenzi ya Mungu.
Sala: Bwana, ninatambua kuwa ulishindwa kueleweka na ukahukumiwa vibaya na
watu wengine, wengine watu wa wakaribu kabisa. Nisaidie daima niweze kukubali
pale ninaposhindwa kueleweka katika maisha hasa pale ninapo kufuata wewe katika
maisha. Nisaidie nikutafute wewe na kufanya mapenzi yako licha ya vipingamizi
kutoka kwa wengine. Yesu, nakuamini wewe. Amina
No comments:
Post a Comment