Everyday Saint / Maisha ya Watakatifu

MASOMO YA MISA, FEBRUARI 1, 2023


MASOMO YA MISA, FEBRUARI 1, 2023
JUMATANO, JUMA LA 4 LA MWAKA WA KANISA

SOMO 1
Ebr. 12;4 – 7, 11 – 15

Hamjafanya vita hata kumwagika damu, mkishindana na dhambi. Tena mmeyasahau yale maonyo, yasemayo nanyi kama kusema na wana, Mwanangu, usiyadharau marudia ya Bwana, wala usizimie moyo ukikemewa naye; maana yeye ambaye Bwana ampenda, humrudi, naye humpiga kil amwana amkubaliye. Ni kwa ajili ya kurudiwa mwastahimi; Mungu awatendea kama wana; maana ni mwana yupi aisyerudiwa na babaye?

Kila adhabu wakati wake haionekani kuwa kitu cha furaha, bali cha huzuni; lakini baadaye huwaletea wao waliozoezwa nayo matunda ya haki yenye Amani. Kwa hiyo inyosheni mikono iliyolegea na magoti yaliyopooza, mkaifanyie miguu yenu njia za kunyoka, ili kitu kilicho kiwete kisipotoshwe, bali afadhali kipnywe.

Tafuteni kwa bidii kuwa na Amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao; mkiangalia kana mtu asiipungukie neema ya Mungu; shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua, na watu wengi wakatiwa unajisi kwa hilo.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.



WIMBO WA KATIKATI
Zab. 103:1 – 2, 13 – 14, 17 – 18

(K) Fadhili za Bwana zina wamchao tangu milele hata milele

Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana
Naam, vyote vilivyo ndani yangu
Vilihimidi jina lake takatifu.
Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana,
Wala usizisahau fadhili zake zote. (K)

Kama vile baba awahurumiavyo watoto wake,
Ndivyo Bwana awahurumia wamchao.
Kwa maana yeye anatujua umbo letu
Na kukumbuka ya kuwa sisi tu mavumbi. (K)

Fadhili za Bwana zina wamchao
Tangu milele na milele,
Na haki yake ina wana wa wana;
Wale washikao agano lake. (K)



SHANGILIO
Yn. 8:12

Aleluya, aleluya,
Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, asema Bwana, yeye anifuataye hatakwenda gizani na kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.
Aleluya.



INJILI
Mk. 6:1-6

Yesu alitoka huko, akafika mpaka nchi ya kwao, wanafunzi wake wakamfuata. Na ilipokuwa sabato, alianza kufundisha katika sinagogi; wengi waliposikia wakashangaa, wakisema, Huyu ameyapata wapi haya? Na, ni hekima gani hii aliyopewa huyu? Na, ni nini miujiza hii mikubwa inayotendeka kwa mikono yake? Huyu si yule seremala, mwana wa Mariamu, na ndugu yao Yakobo, na Yose, na Yuda, na Simoni? Na maumbu yake hawapo hapa petu? Wakajikwaa kwake. Yesu akawaambia, Nabii hakosi heshima, isipokuwa katika nchi yake mwenyewe, na kwa jaama zake, na nyumbani mwake. Wala hakuweza kufanya mwujiza wowote huko; isipokuwa aliweka mikono yake juu ya wagonjwa wachache, akawaponya. Akastaajabu kwa sababu ya kutokuamini kwao.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.



Copyright © 1993 T.M.P. Book Department, Tabora - Tanzania: see MASOMO YA MISA. Scripture readings from ‘Biblia Takatifu’are published and copyright © 1975, 1993 by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania.© Bible Society of Kenya, © Bible Society of Tanzania.These readings are a reproduction by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.

No comments:

Post a Comment