“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya kila siku
Jumanne, Januari 31, 2023
Juma la 4 la Mwaka wa Kanisa
Kumbukumbu ya Mt. Yohane Bosko, Padre
Ebr 12: 1-4;
Zab 22: 26-32;
Mk 5: 21-43
IMANI YA HALI YA JUU!
Katika Injili tunamuona Mwanamke aliyeteseka kwa muda wa miaka kumi na mbili kutokwa na damu. Amejaribu kutibu ugonjwa wake kwa kupitia madaktari mbali mbali na kupoteza karibu kila kitu alichokuwa nacho ili apone, lakini kwa huzuni hakufanikiwa. Inaweza kuwa kweli kwamba Mungu aliruhusu ateseke kwa miaka yote ili aweze kumpa hii nafasi ya pekee ya kudhihirisha Imani yake ili wote waweze kuiona.
“Kama nikigusa pindo la vazi lake tu..” je alitambuaje kwamba atapona? Ni kitu ghani kilicho mwongoza mpaka awe na uhakika wa namna hii? Kwanini, baada ya kupoteza miaka yote kumi na mbili na madaktari mbali mbali na sasa anatambua sasa anaye mhitaji ni Yesu, tena aguse nguo yake apone? Jibu ni rahisi. Ni kwasababu ya zawadi ya Imani yake.
Maelezo haya kuhusu Imani yake yanafunua kwamba Imani ni zawadi ya akili ya hali ya juu ambayo ni Mungu mwenyewe aweza kuifunua. Kwa maneno mengnie, alitambua kwamba atapona, na akili ya Imani hii kwamba atapona ilikuja kwake kwa kupewa na Mungu. Baada ya kupewa alihitajika kuifanyia kazi, kwa kufanya hivyo anatoa ushuhuda wa ajabu kwao wote wanaosoma ujumbee huu siku zote katika Injili. Maisha yake, na yote aliopitia yanapaswa yatupe changamoto tutambue kwamba Mungu anaongea kwa ukweli halisi nasi, kama tutamsikiliza. Kila mara anaongea na kufunua undani wa upendo wake kwetu sisi, akituita tuingie katika maisha ya Imani ya hali ya juu. Anataka Imani yetu isiwe tu msingi wa maisha yetu, bali iwe ushuhuda wa nguvu kwa wengine.
Mwanamke huyu alitambua kuwa Mungu atamponya na akamruhusu aongee naye. Sisi nasi tutafakari kuhusu kusikiliza kwa makini sauti ya Mungu ndani mwetu na kujaribu kuwa wazi kwenye Imani kamili ya ndani kama alivyofanya huyu mwanamke.
Sala: Bwana, nakupenda na natamani kukusikia wewe ukiongea na mimi kila siku. Naomba uongeze Imani yangu ili niweze kukufahamu wewe na mapenzi yako katika maisha yangu. Bwana, nitumie mimi kama upendavyo niweze kuwa shuhuda wa Imani kwa wengine. Yesu, nakutumaini wewe. Amina.
Copyright ©2013-2023 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment