“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya kila siku
Jumatano, Februari 1, 2023
Juma la 4 la Mwaka wa Kanisa
Ebr 12: 4-7;
Zab 103;
Mk 6: 1-6.
MAMBO YA KAWAIDA YANATUFANYA TUWE TAYARI KUPOKEA YASIO YA KAWAIDA!
Watu waliokuwa wanamfahamu Yesu tangu akiwa kijana wanashangazwa na hekima
na mambo makuu anayotenda. Walishangazwa na yote aliokuwa akisema na kutenda.
Walikuwa wakimfahamu tangu alivyokuwa anakuwa, walifahamu wazazi wake na ndugu
wengine, na kwa mshangao wanashangaa inawezekanaje huyu jirani yao wanaye
mfahamu inawezekeanaje awavutie watu hivi na kuwa na hekima ya hali ya juu
namna hii na matendo makuu. Ni wazi kwamba Yesu aliishi maisha ya kawaida kabla
ya kuanza utume wake. Kiasi kwamba watu wake wa karibu hawakufahamu kwamba
alikuwa mtu muhimu sana. Hili ni wazi kwasababu baada ya Yesu kuanza utume wake
wa hadharani watu wake wanashangazwa na matendo yake makuu. Hawakutegemea
kabisa mambo kama haya kutoka kwa Yesu wa “Nazarethi”.
Je, sisi tunaweza kupata nini kutokana na jambo hili? Kwanza kabisa
tutambue , mara nyingi mapenzi ya Mungu kwetu yanatuita kuishi maisha ya
“kawaida” kabisa. Ni rahisi kuwaza kwamba tunapaswa tutende mambo makuu kwa
ajili ya Mungu. Lakini vitu vikubwa ambavyo Mungu anatuitia nikuishi maisha ya
kila siku ya kawaida vizuri. Hakuna wasiwasi kwamba wakati Yesu alivyokuwa
akiishi maisha ya kawaida alikuwa anaishi maisha ya fadhila. Haikuwa mpango wa
Mungu kwanza fadhila zake zianze kujulikana kwanza kwa wote kipindi hicho.
Pili, tunaona wazi kwamba kuna wakati utume wake ulibadilika. Mapenzi ya Baba,
katika maisha yake, alianza utume wake hadharani na watu wakamuona. Na wakati
hili lilivyo anza watu walitambua.
Ukweli huu pia ni dhahiri pia kwetu sisi. Watu wengine wameitwa maisha ya
kawaida katika hali ya kawaida kabisa. Tambua kuwa muda huu ndio muda ulioitwa
ili kukuza fadhila zako, fanya mambo ya kawaida kabisa vizuri, na furahia hali
ya ukimya ya maisha ya kawaida. Pia tutambue kuwa kuna uwezekano Mungu akatuita
katika maisha hayo ya kawaida na kuanza kumshuhudia mbele ya watu au umati.
Ufunguo ni kwamba sisi tunapaswa kumsikiliza na kuitambua sauti yake katika
hali ya utulivu. Kuwa tayari na penda yeye akutumie kwa jinsi alivyopenda kwa
mapenzi yake ya Kimungu.
Leo tutafakari, juu ya mapenzi ya Mungu katika maisha yetu sasa. Anataka
nini kutoka kwetu? Je, anatuita kutoka katika hali yetu ya kawaida ili tuweze
kuishi maisha ya kumshudia yeye mbele za watu? Au anatuita sasa tuishi maisha
ya kawaida katika hali ya ukimya ya kawaida na kupalilia fadhila kwanza?
Furahia mapenzi yake kwa jinsi atakavyo penda uwe na kumbatia hilo kwa moyo
wote.
Sala: Bwana, nakushukuru kwa mpango wako kamili katika maisha yangu.
Ninakushukuru kwa hali mbali mbali ulizoniita ili nikutumikie. Nisaidie daima
niweze kuwa wazi katika mapenzi yako na daima niseme “Ndio” kwako, bila kujali
unataka nifanye nini. Yesu nakuamini wewe. Amina.
No comments:
Post a Comment