“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya kila siku
Jumatatu, Januari 23, 2023
Juma la 3 la Mwaka wa Kanisa
Ebr 9: 15, 24-28;
Zab 98: 1-6;
Mk 3: 22-30.
KUACHA DHAMBI
Leo sehemu ya Injili inatufunulia kuwa kuna dhambi Fulani, dhambi ya
kumkufuru Roho Mtakatifu ambayo haita samehewa. Hii dhambi ni ipi? Kwanini hai
sameheki? Hii ni hali ambayo mtu anatenda dhambi ya mauti na kushindwa
kujisikia hali ya kutotubu na kujiona kama hana kosa au kukataa huruma ya Mungu
inayo muita kufanya toba ya kweli. Hali hii yakuto jisikia kwamba ametenda
dhambi inafunga mlango wakuruhusu huruma ya Mungu. Lakini pia itambulike
kwamba, wakati roho ya mtu inapo badilika na kuonyesha kutubu kwasababu ya
dhambi, Mungu anamkaribisha mara moja mtu huyo kwa mikono miwili. Mungu hawezi
kamwe kumkataa mtu yeyote anaye kwenda kwake kumwomba msamaha kwa moyo mnyofu.
Tutafakari juu ya huruma ya Mungu isio na kikomo, na kutafakari juu ya jukumu
letu la kujinyenyekeza mbele za Mungu tunapokosa. Tutimize jukumu letu kwa moyo
wa unyofu na Mungu atatupa huruma yake. Hakuna dhambi iliyo kubwa kwa Mungu mtu
amwendeapo Mungu kwa moyo mnyofu.
Sala: Bwana, Yesu Kristo, mwana wa Mungu aliye hai, nihurumie mimi mdhambi.
Ninakiri dhambi zangu na ninaomba unisamehe. Nisaidie Bwana wangu, nitazame
ndani mwangu na nijisikie huzuni kwa dhambi zangu na kujikabidhi katika huruma
yako ya Kimungu. Ninakushukuru kwa upendo wako mkamilifu kwangu na kwa wote. Yesu,
nakuamini wewe. Amina.
Copyright ©2013-2023 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki:
see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment