NOVENA YA NOELI SIKU YA TATU
18 Desemba 2022
W: Bwana karibu atafika, Njoni
kumwabudu.
K: Bwana karibu atafika, Njoni
kumwabudu.
W: Furahi, ee binti Sion, na
shangilia sana, ee binti Yerusalem! sikia, Bwana atafika na siku ile utatokea
mwanga mkuu, na milima itatonesha utamu; na vi-lima vitatiririsha maziwa na
asali, kwa sababu atafika nabii mkuu, na Yeye atageuza Yerusalem.
K: Bwana karibu atafika, Njoni kumwabudu.
W: Sasa Mungu-Mtu wa nyumba ya
Daudi atakuja kuketi juu ya kiti cha enzi, mtamwona na moyo wenu utafurahi.
K: Bwana karibu atafika, Njoni
kumwabudu
W: Sikia, atafika Bwana na
Mlinzi wetu, Mtakatifu wa Israel. Kichwani mwake ana taji la ufalme wake:
atatawala nchi toka bahari mpaka bahari, toka mto mpaka ukingoni mwa dunia.
K: Bwana karibu atafika, Njoni
kumwabudu
Sikia, Bwana ataonekana,
hadanganyi hata: akikawia mngoje, kwani atafika tu, hawezi kuchelewa.
K: Bwana karibu atafika, Njoni kumwabudu
Bwana atashuka kama mvua juu ya
ngozi yenye manyoya: katika siku zake kutakuwa na haki na amani tele; na
wafalme wote wa dunia watamwa-budu, na makabila yote yatamtumikia.
K: Bwana karibu atafika, Njoni
kumwabudu
Mtoto atazaliwa kwa ajili yetu
na ataitwa Mungu mwenye nguvu: atakalia kiti cha ezi cha Daudi baba yake;
atatawala, na begani atachukua firhbo ya uwezo wake.
K: Bwana karibu atafika, Njoni
kumwabudu
Ee Bethlehem, mji wa Mungu
mkuu, kwako atatokea Mtawala wa Israel: na uzazi wake ni wa milele, atatukuzwa
katika dunia yote; na atakapofika ita-kuwa amani humu duniani mwetu.
K: Bwana karibu atafika, Njoni
kumwabudu
ZABURI
Mbingu ifurahi nayo dunia
ishangilie,
nanyi mi-lima pigeni
vigelegele.
Milima ionyeshe furaha,
na vilima vitoe haki.
Sababu Bwana wetu atafika,
na atawahurumia maskini wake.
Ee mbingu, nyesheni umande
na mawingu yatuletee
Mtakatifu, nchi ifunguke
na imzae mkombozi.
Utukumbuke, ee Bwana,
na utuletee wokovu wako.
Ee Bwana, utuonyeshe huruma
yako,
nautupe ukombozi wako.
Ee Bwana, umlete Mwana - Kondoo
mfalme wa dunia; atakayetawala toka jiwe la jangwani mpaka mlima wa binti Sion.
Njoo utukomboe, ee Bwana, Mungu
wa Majeshi:
utuonyeshe uso wako na
tutaokoka.
Njoo,
ee Bwana, utuletee amani yako:
ili
tufurahi mbele yako kwa moyo safi.
Tupate
kujua njia yako humu duniani, ee Bwana:
na
tujue wokovu wako katika makabila yote.
Ee
Bwana, amsha nguvu zako na ufike:
ili
utukomboe.
Njoo,
ee Bwana, usikawie:
uliondolee
taifa lako dhambi.
Ee,
laiti ungepasua mbingu na kushuka:
milima
ingeyeyuka mbele yako.
Njoo,
ee Bwana, utuonyeshe uso wako:
wewe
unayeketi juu ya Malaika.
Atukuzwe Baba, na Mwana, na
Roho Mtakatifu
kama mwanzo na sasa na siku
zote na milele. Amina.
WIMBO WA BIKIRA MARIA
K: Ee Adonai, na Kiongozi wa
nyumba ya Israeli, uli-yejionyesha kwa Moise katika kichaka chenye kuwaka: na
uliyempa sheria mlimani Sinai, njoo utukomboe kwa ezi ya mkono wako.
Moyo wangu wamtukuza Bwana,
Roho yangu inafurahi
kwa sababu ya Mungu Mwokozi wangu.
Kwa kuwa amemwangalia kwa
huruma,
mtumishi wake mdogo,
Hivyo tangu sasa watu wote
wataniita mwenye heri.
Kwa kuwa Mwenyezi Mungu
amenitendea makuu,
jina lake ni takatifu.
Huruma yake kwa watu wanaomcha
hudumu
kizazi hata kizazi.
Amefanya
mambo makuu kwa mkono wake:
amewatawanya
wenye kiburi katika mawazo ya mioyo yao;
amewashusha
wenye nguvu kutoka vitu vyao vya enzi,
akawakweza
wanyenyekevu.
Wenye
njaa amewashibisha mema,
matajiri amewaacha waende
mikono mitupu.
Amempokea Israeli mtumishi wake,
akikumbuka huruma yake.
Kama alivyowaahidia wazee wetu,
Abrahamu na uzao wake hata
milele.
K: Ee Adonai, na Kiongozi wa
nyumba ya Israeli, uli-yejionyesha kwa Moise katika kichaka chenye kuwaka: na
uliyempa sheria mlimani Sinai, njoo utukomboe kwa ezi ya mkono wako.
Sala:
Ee Bwana twakusihi uharikishe wala usichelewe na utuletee nguvu ya juu, kusudi
wote wanaotumainia huruma yako wapate kufariji wana majilio yako, unayeishi na
kutawala milele. Amina.
No comments:
Post a Comment