“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Alhamisi, Desemba 22, 2022
Juma la 4 la Majilio
1 Sam 1: 24-28;
1 Sam 2: 1, 4-8;
Lk 1: 46-56
MSIFU MUNGU KILA WAKATI!
Wimbo wa Maria unapaswa kulinganishwa na ule wa
Hanna (1 Sam 2: 1-10) na Zakaria (Lk 1: 68-79). Wimbo huu unafunua furaha ya
moyo wa Mama wa Mungu. Anakiri mambo makuu aliomtendea Mungu na anaelezea
furaha yake ya ndani. Ni vizuri kuona kwamba “moyo” wake na “roho” yake
vinafuraha. Vinaelezea matendo yake na matendo ya Mungu. Moyo wa Mama yetu
mbarikiwa vinaelezea uwezo wake wa kibinadamu katika akili yake, hisia na
matamanio. Hivi ndivyo vinamfanya binadamu. Na katika hali hiyo ya kibinadamu
anatangaza ukuu wa Mungu. Kwa maneno mengine, kwa akili yake aliweza kuhisi
ukuu wa Mungu, na hivyo anachagua kuutukuza na kuutangaza ukuu wa Mungu na
anafanya hivyo kwa hisia zake zote. Utu wake wote ulimezwa na ukuu wa Mungu.
Wakati unabii wa Maria ukisimama katika hali
mbalimbali, utofauti wake mkubwa ni katika maana zake. Hanna anamsifu Mungu kwa
kumtoa Samueli. Alikuwa katika aibu ya kuwa mgumba (1 Sam 1: 7). Kuzaliwa kwa
Samueli kumebadilisha yote hayo, na ana sababu ya kumsifu Mungu. Kadhalika,
Zakaria amevumilia kwa muda wa miaka mingi bila kuwa na mtoto na kuwa bubu kwa
miezi tisa (Lk 1: 20, 62). Na sasa mtoto wake amezaliwa, na ulimi wake
ukafunguliwa, (Lk 1: 64), na ana kila sababu ya kumsifu Mungu. Kwa
kulinganisha, tunaona Luka anaweka, sifa za Maria mwanzoni kabisa mwa mimba
yake. Alikuwa anamsifu Mungu sio baada tu ya mateso lakini kabla na wakati wa
mateso. Alikuwa akisifu katika hali zote. Alikuwa akisifu kwa Imani na sio
kwasababu ameona jambo fulani (2 Cor 5: 7).
Je, mimi na wewe tunaiga huu mfano kamili wa Mama
yetu mbarikiwa, kama alivyo tafuta kufahamu, kupenda na kutangaza ukuu wa Mungu
kwa mwili wake wote? Je, unaruhusu roho Mtakatifu kufurisha moyo wako na
furaha? Tuombee kwa ajili ya neema ya Mungu “tutangaze” na “tufurahi” pamoja
naye anapozaliwa Mwana wa Mungu, ili wewe pia uweze kuimba wimbo wa furaha!
Sala: Mama mpendwa, ulionesha mfano kamili wa
jinsi ya kuishi kwa Imani na uaminifu na unyenyekevu wa mtumishi wa Mungu aliye
juu. Ulitangaza ukuu wake na ulijazwa na furaha ya kuja kwake. Nisaidie mimi,
kwa maombezi yako yenye nguvu, niweze kuiga Imani yako, kumpenda Mungu kwa moyo
wangu wote. Mama Maria niombee mimi. Yesu nakutumainia wewe. Amina
Copyright ©2013-2022 ©FurKat, Furaha ya
Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment