NOVENA YA NOELI,
SIKU YA NANE
23 Desemba 2022
W: Bwana karibu atafika, Njoni kumwabudu.
K: Bwana karibu atafika, Njoni kumwabudu.
W: Furahi, ee binti Sion, na shangilia sana, ee binti Yerusalem! sikia, Bwana atafika na siku ile utatokea mwanga mkuu, na milima itatonesha utamu; na vi-lima vitatiririsha maziwa na asali, kwa sababu atafika nabii mkuu, na Yeye atageuza Yerusalem.
K: Bwana karibu atafika, Njoni kumwabudu.
W: Sasa Mungu-Mtu wa nyumba ya Daudi atakuja kuketi juu ya kiti cha enzi, mtamwona na moyo wenu utafurahi.
K: Bwana karibu atafika, Njoni kumwabudu
W: Sikia, atafika Bwana na Mlinzi wetu, Mtakatifu wa Israel. Kichwani mwake ana taji la ufalme wake: atatawala nchi toka bahari mpaka bahari, toka mto mpaka ukingoni mwa dunia.
K: Bwana karibu atafika, Njoni kumwabudu
Sikia, Bwana ataonekana, hadanganyi hata: akikawia mngoje, kwani atafika tu, hawezi kuchelewa.
K: Bwana karibu atafika, Njoni kumwabudu
Bwana atashuka kama mvua juu ya ngozi yenye manyoya: katika siku zake kutakuwa na haki na amani tele; na wafalme wote wa dunia watamwa-budu, na makabila yote yatamtumikia.
K: Bwana karibu atafika, Njoni kumwabudu
Mtoto atazaliwa kwa ajili yetu na ataitwa Mungu mwenye nguvu: atakalia kiti cha ezi cha Daudi baba yake; atatawala, na begani atachukua firhbo ya uwezo wake.
K: Bwana karibu atafika, Njoni kumwabudu
Ee Bethlehem, mji wa Mungu mkuu, kwako atatokea Mtawala wa Israel: na uzazi wake ni wa milele, atatukuzwa katika dunia yote; na atakapofika ita-kuwa amani humu duniani mwetu.
K: Bwana karibu atafika, Njoni kumwabudu
ZABURI
Mbingu ifurahi nayo dunia ishangilie,
nanyi milima pigeni vigelegele.
Milima ionyeshe furaha,
na vilima vitoe haki.
Sababu Bwana wetu atafika,
na atawahurumia maskini wake.
Ee mbingu, nyesheni umande
na mawingu yatuletee
Mtakatifu, nchi ifunguke
na imzae mkombozi.
Utukumbuke, ee Bwana,
na utuletee wokovu wako.
Ee Bwana, utuonyeshe huruma yako,
nautupe ukombozi wako.
Ee Bwana, umlete Mwana - Kondoo mfalme wa dunia; atakayetawala toka jiwe la jangwani mpaka mlima wa binti Sion.
Njoo utukomboe, ee Bwana, Mungu wa Majeshi:
utuonyeshe uso wako na tutaokoka.
Njoo, ee Bwana, utuletee amani yako:
ili tufurahi mbele yako kwa moyo safi.
Tupate kujua njia yako humu duniani, ee Bwana:
na tujue wokovu wako katika makabila yote.
Ee Bwana, amsha nguvu zako na ufike:
ili utukomboe.
Njoo, ee Bwana, usikawie:
uliondolee taifa lako dhambi.
Ee, laiti ungepasua mbingu na kushuka:
milima ingeyeyuka mbele yako.
Njoo, ee Bwana, utuonyeshe uso wako:
wewe unayeketi juu ya Malaika.
Atukuzwe Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu
kama mwanzo na sasa na siku zote na milele. Amina.
WIMBO WA BIKIRA MARIA
K: Ee Emanuel, Mfalme na mtawala wetu, mngoje wana mataifa na Mkombozi wao; uje utukomboe, ee Bwana Mungu wetu.
Moyo wangu wamtukuza Bwana,
Roho yangu inafurahi
kwa sababu ya Mungu Mwokozi wangu.
Kwa kuwa amemwangalia kwa huruma,
mtumishi wake mdogo,
Hivyo tangu sasa watu wote wataniita mwenye heri.
Kwa kuwa Mwenyezi Mungu amenitendea makuu,
jina lake ni takatifu.
Huruma yake kwa watu wanaomcha
hudumu kizazi hata kizazi.
Amefanya mambo makuu kwa mkono wake:
amewatawanya wenye kiburi katika mawazo ya mioyo yao;
amewashusha wenye nguvu kutoka vitu vyao vya enzi,
akawakweza wanyenyekevu.
Wenye njaa amewashibisha mema,
matajiri amewaacha waende mikono mitupu.
Amempokea Israeli mtumishi wake,
akikumbuka huruma yake.
Kama alivyowaahidia wazee wetu,
Abrahamu na uzao wake hata milele.
K: Ee Emanuel, Mfalme na mtawala wetu, mngoje wana mataifa na Mkombozi wao; uje utukomboe, ee Bwana Mungu wetu.
Sala: Ee Bwana twakusihi uharikishe wala usichelewe na utuletee nguvu ya juu, kusudi wote wanaotumainia huruma yako wapate kufariji wana majilio yako, unayeishi na kutawala milele. Amina.
No comments:
Post a Comment