Everyday Saint / Maisha ya Watakatifu

MASOMO YA MISA, DESEMBA 22, 2022


MASOMO YA MISA, DESEMBA 22, 2022
ALHAMISI, JUMA LA 4 LA MAJILIO



SOMO 1
1 Sam. 1:24 – 28

Siku zile, hana alimchukua Samweli pamoja naye, na ng’ombe watatu, na efa moja ya unga, na chupa ya divai, akamleta nyumbani kwa Bwana, huko Shilo; na yule mtoto alikuwa mtoto mdogo. Nao wakamchinja huyo ng’ombe, wakamleta mtoto kwa Eli.

Hana akasema, Ee Bwana wangu, kama iishivyo roho yako, bwana wangu, mimi ndimi yule mwanamke aliyesimama karibu nawe hapa, nikimwomba Bwana. Naliomba nipewe mtoto huyu; Bwana akanipa dua yangu niliyomwomba; kwa sababu hiyo mimi nami nimempa Bwana mtoto huyu; wakati wote atakaokuwa hai amepewa Bwana. Naye akamwabudu Bwana huko.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.



WIMBO WA KATIKATI
1 Sam. 2:1, 4 – 8 (K) 1

(K) Moyo wangu wamshangilia Bwana Mwokozi wangu.

Moyo wangu wamshangilia Bwana,
Pembe yangu imetukuka katika Bwana.
Kinywa changu kimepanuka juu ya adui zangu;
Kwa kuwa naufurahia wokovu wako. (K)

Pinde zao mashujaa zimevunjika,
Na hao waliojikwa wamefungiwa nguvu.
Walioshiba wamejikodisha ili kupata chakula,
Na hao waliokuwa na njaa wamepata raha.
Naam, huyo aliyekuwa tasa amezaa watoto saba,
Na yeye aliye na wana wengi amedhoofika. (K)

Bwana huua, naye hufanya watu hai;
Hushusha hata kuzimu, tena huleta juu.
Bwana hufurahisha mtu, naye hutajirisha;
Hushuhsa chini, tena huinua juu. (K)

Humwinua mnyonge kutoka mavumbini,
Humpandisha mhitaji kutoka jaani,
Ili awaketishe pamoja na wakuu,
Wakakirithi kiti cha enzi cha utukufu. (K)



SHANGILIO
Aleluya, aleluya,
Ee Mfalme wa mataifa na jiwe la msingi wa Kanisa uje kumwokoa mwanadamu aliyemuumba kwa udongo.
Aleluya.



INJILI
Lk. 1:46 – 56

Sik ile Maria alisema: Moyo wangu wamwadhimisha Bwana, na roho yangu imemfurahia Mungu, Mwokozi wangu; kwa kuwa ameutazama unyonge wa mjakazi wake. Kwa maana, tazama, tokea sasa vizazi vyote wataniita mbarikiwa; kwa kuwa mwenye nguvu amenitendea makuu, na jina lake ni takatifu. Na rehema zake hudumu vizazi hata vizazi kwa hao wanaomcha. Amefanya nguvu kwa mkono wake; amewatawanya walio na kiburi katiak mawazo ya mioyo yao; amewaangusha wakuu kati aviti vyao vya enzi; na wanyonge amewakweza. Wenye njaa amewashibisha mema, na wenye mali amewaondoa mikono mitupu. Amemsaidia Israeli, mtumishi wake; ili kukumbuka rehema zake; kama alivyowaambia baba zetu, Ibrahimu na uzao wake hata milele.

Mariamu akakaa naye kadiri ya miezi mitatu kisha akarudi kwenda nyumbani mwake.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.


Copyright © 1993 T.M.P. Book Department, Tabora - Tanzania: see MASOMO YA MISA. Scripture readings from ‘Biblia Takatifu’are published and copyright © 1975, 1993 by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania.© Bible Society of Kenya, © Bible Society of Tanzania.These readings are a reproduction by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.

No comments:

Post a Comment