“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Alhamisi, Novemba 17, 2022
Juma la 33 la Mwaka wa Kanisa
Ufu 5:1-10;
Zab 149:1-6, 9;
Lk 19:41-44
JE, TUNAPATA UTUKUFU KATIKA YERUSALEMU YA ZAMANI
AU KATIKA YERUSALEMU MPYA?
Mji wa Yerusalemu, na hekalu lake, ilikuwa ni
alama ya dini ya Wayahudi, na kila Myahudi alijitambulisha kwa kutumia alama
hiyo. Yesu, anatamani kufikisha ujumbe wake kwa wafuasi wake kwamba, sio Hekalu
la duniani la mji wa Yerusalemu walilokuwa wakisemea manabii, bali Yerusalemu
mpya, mji wa kiroho wa utawala wa Mungu. Somo la kwanza kutoka katika kitabu
cha Ufunuo linaongelea kuhusu mji huu mpya wa Yerusalemu. Mwana-kondoo (Yesu
Mwenyewe) kwa kumwaga damu yake, amewaokoa na kujipatia watakatifu wengi wa Mungu
kutoka katika kila taifa, na sasa wanatawala katika Ufalme wa Mungu, Yerusalemu
mpya. Je, unataka kuwa katika Yerusalemu ipi?
Sala: Bwana, nisadie
nisipoteze macho yakutazama Yerusalemu mpya ulio iandaa kwa ajili yangu. Amina
No comments:
Post a Comment