MASOMO YA MISA, OKTOBA 9,
JUMAPILI, 2022
DOMINIKA YA 28 YA MWAKA C WA KANISA
SOMO LA 1
2 Fal 5:14-17
Naamani
alishuka, akajichovya mara saba katika Yordani, sawasawa na neno lake yule mtu
wa Mungu; nayo nyama ya mwili wake ikarudi ikawa kama nyama ya mwili wa mtoto
mchanga, akawa safi. Akamrudia yule mtu wa Mungu, yeye na mafuatano yake yote.
Akaja, akasimama mbele yake; akasema, Sasa tazama, najua ya kwamba hakuna Mungu
duniani mwote, ila katika Israeli; basi nakuomba upokee mbaraka kwa mtumwa
wako. Lakini akasema, Kama Bwana aishivyo, ambaye nimesimama mbele yake,
sipokei kitu. Akamshurutisha apokee; lakini akakataa. Naamani akasema; Kama
sivyo, lakini mtumwa wako na apewe mzigo wa udongo wa baghala wawili; kwa maana
mtumwa wako hatatoa tena sadaka ya kuteketezwa wala dhabihu kwa miungu mingine,
ila kwa Bwana.
Neno la Bwana………..Tumshukuru
Mungu.
WIMBO WA KATIKATI
Zab 98:1-4
Mwimbieni
Bwana wimbo mpya,
Kwa
maana ametenda mambo ya ajabu.
Mkono
wa kuume wake wenyewe,
Mkono
wake mtakatifu umetenda wokovu
(K)
Bwana ameufunua wokovu wake machoni pa mataifa
Bwana
ameufunua wokovu wake,
Machoni
pa mataifa ameidhihirisha haki yake
(K)
Bwana ameufunua wokovu wake machoni pa mataifa
Miisho
yote ya dunia imeuona wokovu wa Mungu wetu,
Mshangilieni
Bwana, nchi yote. Inueni sauti, imbeni kwa furaha
(K)
Bwana ameufunua wokovu wake machoni pa mataifa
SOMO LA 2
2 Tim 2:8-13
Mkumbuke
Yesu Kristo, aliyefufuka katika wafu, wa uzao wa Daudi kama inenavyo injili
yangu. Nami katika hiyo nimeteswa hata kufungwa kama mtenda mabaya; lakini neno
la Mungu halifungwi. Kwa ajili ya hilo nastahimili mambo yote, kwa ajili ya
wateule, ili wao nao waupate wokovu ule ulio katika Kristo Yesu, pamoja na
utukufu wa milele. Ni neno la kuaminiwa. Kwa maana, Kama tukifa pamoja naye,
tutaishi pamoja naye pia; Kama tukistahimili, tutamiliki pamoja naye; Kama
tukimkana yeye, yeye naye atatukana sisi; Kama sisi hatuamini, yeye hudumu wa
kuaminiwa. Kwa maana hawezi kujikana mwenyewe.
Neno la Bwana……………….Tumshukuru
Mungu.
SHANGILIO
Yn 10:27
Aleluya,
aleluya
Kondoo
wangu waisikia sauti yangu, asema Bwana: Nami nawajua nao wanifuata.
Aleluya
INJILI
Lk 17:11-19
Yesu
alipokwenda njiani kwenda Yerusalemu, alikuwa akipita katikati ya Samaria na
Galilaya. Na alipoingia katika kijiji kimoja, alikutana na watu kumi wenye
ukoma; wakasimama mbali, wakapaza sauti wakisema, Ee Yesu, Bwana mkubwa,
uturehemu! Alipowaona aliwaambia, Enendeni, mkajionyeshe kwa makuhani. Ikawa
walipokuwa wakienda walitakasika. Na mmoja wao alipoona kwamba amepona,
alirudi, huku akimtukuza Mungu kwa sauti kuu; akaanguka kifudifudi miguuni
pake, akamshukuru; naye alikuwa Msamaria. Yesu akajibu, akanena, Hawakutakaswa
wote kumi? Wale kenda wa wapi? Je! Hawakuonekana waliorudi kumpa Mungu utukufu
ila mgeni huyu? Akamwambia, Inuka, enenda zako, imani yako imekuokoa.
Neno la Bwana………………Sifa kwako Ee
Kristo
Copyright
© 1993 T.M.P. Book Department, Tabora - Tanzania: see MASOMO YA MISA. Scripture
readings from ‘Biblia Takatifu’are published and copyright © 1975, 1993 by
T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania.© Bible Society of Kenya, © Bible
Society of Tanzania.These readings are a reproduction by Furaha ya Kikatoliki:
see www.fur-kat.blogspot.com.
Asante Kwa masomo ya Misa Leo.
ReplyDelete