“MBEGU ZA UZIMA”
Jumapili,
Oktoba 9, 2022
Juma la
28 la Mwaka C wa Kanisa
2 Fal
5: 14-17;
Zab 98:
1-4;
2 Tim
2: 8-13;
Lk 17:
11-19
KUTOKA
KWENYE UPONYA HADI KWENYE IMANI
Injili
ya Leo inaongelea kuhusu Msamaria aliye na shukrani aliyeponywa. Walio wengi
wanachukua kipengele hiki cha Injili kama somo la mtu mwenye tabia njema,
kukumbuka kusema "asante,". Msamaria huyu aliye ponywa ukoma wake
anamshangaza Yesu. Msamaria huyu alikuwa na maono ya Kimungu, ambayo wale
Wayahudi tisa, walio elimishwa katika imani na kukubali maandiko, hawakuwa
nayo. Ingawaje wote kumi walijua kwamba Yesu alikuwa mponyaji. Mwanga mpya
uliingarisha tu akili na moyo wa Msamaria yule. Alitambua kuwa Yesu alikuwa
zaidi ya mponyaji. Katika harakati za ukombozi wake mkoma huyu alifanikiwa
kunasa ujumbe wa Mungu. Huyu ambaye hakuwa anawaamini manabii, anashangaza
kwamba anatambua kuwa ni Mungu aliyemtuma, yeye ambaye manabii walimtangaza. Ni
yeye wa kwanza kutambua Mungu hayupo mbali na wakoma. Kwa njia ya Kristo,
Mungu, alitoka katikati yao; anawagusa na kuwaponya.
Somo la
kwanza linaongelea kuhusu Naaman, Kamanda wa majeshi, alikuwa na ukoma. Kwa
amri ya neno la Elisha, Naaman anaenda kujichovia katika mto Yordani,
anajichovia Mara saba na hatimaye ngozi yake inarudi na kuwa kama ya mtoto
mchanga, aliponywa. Anarudi kumshukuru Elisha akiwa na zawadi lakini Elisha
anaikataa zawadi. Uponyaji haupaswi kuelekezwa kwake, bali kwa Mungu. Naaman
anatambua na anamtukuza Mungu “sasa natambua hakuna Mungu mwingine duniani ila
Mungu wa Israeli” ( mstari wa 15-16. ) kuanzia sasa sinta mwabudu Mungu
mwingine isipokuwa Bwana”. Naaman anaponywa si tu ukoma bali roho yake. Kutoka
kwenye upagani anaingia kwenye Imani ya kweli ya Mungu mmoja.
Wakati
Paulo anaandika barua ya pili kwa Timotheo, alikuwa gerezani, Rumi. Alikuwa
tayari ameshachukua hatua ya kwanza lakini hakuna hata mmoja aliyekuwa na nguvu
ya kutoa ushuhuda juu yake ili kumtetea (2 Tim 4:16). Marafiki wengi walimtenga
na wakawa mstari wa mbele kumpinga (2 Tim 4:9-15). Kinacho wapa faraja mitume
kipindi hiki cha magumu ni kwamba Kristo pia alipitia mateso mengi na
kutokueleweka kabla ya kuingia katika utukufu wa Baba yake! Kwa hili anamwambia
Timotheo na anajiambia mwenyewe; “Mkumbuke Yesu Kristo” (2Tim2: 8). Kupitia
ukombozi ni muhimu kupitia njia hiyo hiyo. “Kama tutakufa pamoja naye, tutaishi
pia pamoja naye”. Kama tutavumilia pamoja naye, tutatukuka pamoja naye (2 Tim.
11-12). Yaliotokea kwa Yesu na Paulo yanaturidiwa kwa kila mfuasi mwaminifu wa
Kristo.
Katika
kipindi cha Yesu kuna aina nne za watu waliochukuliwa kama watu waliokufa au
wasioshi: maskini, wakoma, vipofu na wasio na watoto. Magonjwa yote
yalichukuliwa kuwa adhabu kwasababu ya dhambi, lakini ukoma ulichukuliwa kuwa
ndio alama ya dhambi yenyewe. Muujiza wa kumponya mtu aliyekuwa na ukoma
ilikuwa ni sawa na muujiza wa kumfufua mtu kutoka wafu. Ni Bwana mwenyewe
aliyeweza kuuponya. Ujumbe katika Injili hauelezei mkoma mmoja tu bali wakoma
kumi. Namba kumi katika Biblia ina thamani: ina maanisha ukamilifu (ujumla)
(mikono ina vidole kumi). Wakoma katika Injili wanawakilisha watu wote,
ubinadamu wote walio mbali na Mungu. Sisi wote-Luka anataka kutuambia ni wakoma
na tunahitaji kukutana na Yesu. Hakuna hata mmoja wetu aliye mkamilifu, sisi
wote tumebeba ngozi alama ya kifo ambapo ni Yesu mwenyewe anaweza kutuponya.
Kila anayejitambua mwenyewe kwamba ni mkoma hawezi kujiona mwenye nguvu, hawezi
kuhukumu, hawezi kujitenga, wala kuona haya nakutazama chini, bali tutakuwa
katika mshikamano katika mema na mabaya kama kaka na dada.
Katika
ujumbe wa Injili unasema kwamba ni Msamaria pekee aliyempa Mungu utukufu, ni
yeye mwenyewe aliyetambua kuwa ukombozi wa Mungu umekuja kwa watu kupitia
Kristo. Ni yeye aliyekiri mema aliyepokea na pia kutambua amachaguliwa na Mungu
kufikisha ujumbe wa zawadi aliopewa na Mungu. Anatamani kuitangza kwao wote,
kwa shukrani na moyo wakujitambua. Wale wengine waliridhika na uponyaji wa
mwili, lakini Msamaria huyu aliyekuwa mkoma na kama Naaman walipokea uponyaji
na kuingia katika Imani. Walipokea zawadi ya ukombozi. Sisi ni wakoma
tuliojitenga mbali na ukombozi na huruma ya Mungu kwa njia ya kuanguka kwetu na
dhambi zetu. Tuombe uponyaji wa Imani, tamaa ya kupokea huruma ya Mungu na hasa
zaidi katika mwaka huu wa huruma ya Mungu na daima katika maisha yetu yote.
Sala:
Bwana Yesu, naomba uniwezeshe niweze kutambua kazi yako ya ukombozi katika
maisha yangu. Amina
Copyright
©2013-2022 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com
Amina
ReplyDelete