Everyday Saint / Maisha ya Watakatifu

KUTOKA KWENYE UPONYA HADI KWENYE IMANI




























 “MBEGU ZA UZIMA”
Jumapili, Oktoba 9, 2022
Juma la 28 la Mwaka C wa Kanisa

2 Fal 5: 14-17;
Zab 98: 1-4;
2 Tim 2: 8-13;
Lk 17: 11-19


KUTOKA KWENYE UPONYA HADI KWENYE IMANI

Injili ya Leo inaongelea kuhusu Msamaria aliye na shukrani aliyeponywa. Walio wengi wanachukua kipengele hiki cha Injili kama somo la mtu mwenye tabia njema, kukumbuka kusema "asante,". Msamaria huyu aliye ponywa ukoma wake anamshangaza Yesu. Msamaria huyu alikuwa na maono ya Kimungu, ambayo wale Wayahudi tisa, walio elimishwa katika imani na kukubali maandiko, hawakuwa nayo. Ingawaje wote kumi walijua kwamba Yesu alikuwa mponyaji. Mwanga mpya uliingarisha tu akili na moyo wa Msamaria yule. Alitambua kuwa Yesu alikuwa zaidi ya mponyaji. Katika harakati za ukombozi wake mkoma huyu alifanikiwa kunasa ujumbe wa Mungu. Huyu ambaye hakuwa anawaamini manabii, anashangaza kwamba anatambua kuwa ni Mungu aliyemtuma, yeye ambaye manabii walimtangaza. Ni yeye wa kwanza kutambua Mungu hayupo mbali na wakoma. Kwa njia ya Kristo, Mungu, alitoka katikati yao; anawagusa na kuwaponya.

Somo la kwanza linaongelea kuhusu Naaman, Kamanda wa majeshi, alikuwa na ukoma. Kwa amri ya neno la Elisha, Naaman anaenda kujichovia katika mto Yordani, anajichovia Mara saba na hatimaye ngozi yake inarudi na kuwa kama ya mtoto mchanga, aliponywa. Anarudi kumshukuru Elisha akiwa na zawadi lakini Elisha anaikataa zawadi. Uponyaji haupaswi kuelekezwa kwake, bali kwa Mungu. Naaman anatambua na anamtukuza Mungu “sasa natambua hakuna Mungu mwingine duniani ila Mungu wa Israeli” ( mstari wa 15-16. ) kuanzia sasa sinta mwabudu Mungu mwingine isipokuwa Bwana”. Naaman anaponywa si tu ukoma bali roho yake. Kutoka kwenye upagani anaingia kwenye Imani ya kweli ya Mungu mmoja.

Wakati Paulo anaandika barua ya pili kwa Timotheo, alikuwa gerezani, Rumi. Alikuwa tayari ameshachukua hatua ya kwanza lakini hakuna hata mmoja aliyekuwa na nguvu ya kutoa ushuhuda juu yake ili kumtetea (2 Tim 4:16). Marafiki wengi walimtenga na wakawa mstari wa mbele kumpinga (2 Tim 4:9-15). Kinacho wapa faraja mitume kipindi hiki cha magumu ni kwamba Kristo pia alipitia mateso mengi na kutokueleweka kabla ya kuingia katika utukufu wa Baba yake! Kwa hili anamwambia Timotheo na anajiambia mwenyewe; “Mkumbuke Yesu Kristo” (2Tim2: 8). Kupitia ukombozi ni muhimu kupitia njia hiyo hiyo. “Kama tutakufa pamoja naye, tutaishi pia pamoja naye”. Kama tutavumilia pamoja naye, tutatukuka pamoja naye (2 Tim. 11-12). Yaliotokea kwa Yesu na Paulo yanaturidiwa kwa kila mfuasi mwaminifu wa Kristo.

Katika kipindi cha Yesu kuna aina nne za watu waliochukuliwa kama watu waliokufa au wasioshi: maskini, wakoma, vipofu na wasio na watoto. Magonjwa yote yalichukuliwa kuwa adhabu kwasababu ya dhambi, lakini ukoma ulichukuliwa kuwa ndio alama ya dhambi yenyewe. Muujiza wa kumponya mtu aliyekuwa na ukoma ilikuwa ni sawa na muujiza wa kumfufua mtu kutoka wafu. Ni Bwana mwenyewe aliyeweza kuuponya. Ujumbe katika Injili hauelezei mkoma mmoja tu bali wakoma kumi. Namba kumi katika Biblia ina thamani: ina maanisha ukamilifu (ujumla) (mikono ina vidole kumi). Wakoma katika Injili wanawakilisha watu wote, ubinadamu wote walio mbali na Mungu. Sisi wote-Luka anataka kutuambia ni wakoma na tunahitaji kukutana na Yesu. Hakuna hata mmoja wetu aliye mkamilifu, sisi wote tumebeba ngozi alama ya kifo ambapo ni Yesu mwenyewe anaweza kutuponya. Kila anayejitambua mwenyewe kwamba ni mkoma hawezi kujiona mwenye nguvu, hawezi kuhukumu, hawezi kujitenga, wala kuona haya nakutazama chini, bali tutakuwa katika mshikamano katika mema na mabaya kama kaka na dada.

Katika ujumbe wa Injili unasema kwamba ni Msamaria pekee aliyempa Mungu utukufu, ni yeye mwenyewe aliyetambua kuwa ukombozi wa Mungu umekuja kwa watu kupitia Kristo. Ni yeye aliyekiri mema aliyepokea na pia kutambua amachaguliwa na Mungu kufikisha ujumbe wa zawadi aliopewa na Mungu. Anatamani kuitangza kwao wote, kwa shukrani na moyo wakujitambua. Wale wengine waliridhika na uponyaji wa mwili, lakini Msamaria huyu aliyekuwa mkoma na kama Naaman walipokea uponyaji na kuingia katika Imani. Walipokea zawadi ya ukombozi. Sisi ni wakoma tuliojitenga mbali na ukombozi na huruma ya Mungu kwa njia ya kuanguka kwetu na dhambi zetu. Tuombe uponyaji wa Imani, tamaa ya kupokea huruma ya Mungu na hasa zaidi katika mwaka huu wa huruma ya Mungu na daima katika maisha yetu yote.

Sala: Bwana Yesu, naomba uniwezeshe niweze kutambua kazi yako ya ukombozi katika maisha yangu. Amina


Copyright ©2013-2022 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com

1 comment: