Everyday Saint / Maisha ya Watakatifu

KUWA WA KWANZA!


“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Jumamosi, Oktoba 29, 2022
Juma la 30 la Mwaka wa Kanisa

Flp 1: 18-26;
Zab 42: 2-3, 5;
Lk 14: 1, 7-11


KUWA WA KWANZA!

Wana michezo mashuhuri walisema; “kushinda sio kila kitu, ni kitu tu”. Kwa maneno mengine, kuwa wakwanza ni muhimu sana kwa wengine kiasi kwamba inakuwa ndicho kitu pekee anacho shughulikia. Hakuna kingine tena kinacho kubalika. Lakini kwa Mkristo kuna utofauti kati ya tamaa yake na mafundisho ya Kristo anayemfuata. Yesu alisema “Kama mmoja akitaka kuwa wakwanza, anapaswa kuwa wa mwisho na mtumishi wa wote.” (Mk 9: 35). Je, tunaona tofauti katika maana? Wana michezo wanatuambia “tuwe wa kwanza” Bwana wetu anatuambia “tuwe wamwisho”. Wote wanatuelekeza ni jinsi ghani ya kufika juu, lakini tofauti ya maana ni kama usiku na mchana.

Jambo ambalo Yesu anataka kutuambia ni kwamba unyenyekevu ni alama muhimu sana katika Ufalme wake. Je, sisi ni moja wapo wa watu wenye majivuno au wanyenyekevu? Yesu anazungumza nasi leo na anasema “atakaye jikweza mwenyewe atashushwa. Na wote wanao jinyenyekesha wenyewe watakwezwa.”

Barua ya Mt. Paulo kwa Wafilipi inaelezea furaha ya Paulo katika mateso. Furaha ya Paulo ilikuwa kwamba kwa njia ya mateso yake na mateso ya Wafilipi wote, Injili iweze kukuwa na kuenea. Inatueleza sisi pia kwamba pamoja kwamba kuhubiri Injili ilikuwa ndio kazi kuu ya Paulo, hakujikweza na kujivuna kwa mafanikio ya Injili. Mungu asipotupa neema ya kutambua na kuona majivuno yetu ndani yetu twaweza kuishia hata katika kushindana katika kuhubiri Injili tukiongozwa na mitizamo mibaya.

Unyenyekevu kwa njia nyingine ni kujitambua sisi ni nani. Unaanza kwakumtambua Mungu kama chanzo na lengo la maisha yetu. Alafu, kutumia vipaji vyote vinavyo tutambulisha kuwa sisi ni wanani, na mwishowe, kutumia vipaji hivi kutoka kwa Mungu kwa kumpa utukufu yeye na kuwasaidia ndugu zetu wote kama wanadamu.

Sala: Bwana, nipe neema ya kutambua majivuno ndani mwangu na naomba unipe neema ya kuwa mnyenyekevu. Amina


Copyright ©2013-2022 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com

No comments:

Post a Comment