MASOMO YA MISA, JUNI 9, 2026
JUMANNE, JUMA LA 10 LA MWAKA
SOMO 1
l Fal. 17:7-16
Baada ya siku kupita, kite kijito kikakauka, kwa sababu mvua haikunya katika nchi. Neno la Bwana likamjia Eliya, kusema, Ondoka, uende Sarepta, ulio mji wa Sidoni, ukae huko. Tazama, nimemwagiza mwanamke mjane wa huko akulishe. Basi, akaondoka, akaenda Sarepta; hata alipofika langoni pa mji, kumbe! mwanamke mjane alikuwako akiokota kuni; akamwita, akamwambia, Niletee, nakuomba, maji kidogo chomboni nipate kunywa.
Alipokuwa akienda kuleta, akamwita akasema, Niletee, nakuomba, kipande cha mkate mkononi
mwako. Naye akasema, Kama Bwana, Mungu wako, aishivyo, sina mkate, ila konzi ya unga katika pipa, na mafuta kidogo katika chupa; nami ninaokota kuni mbili ili nilngie nijipikie nafsi yangu na mwanangu, tuule tukafe.
Eliya akamwambia, Usiogope; enenda ukafanye kama ulivyosema; lakini unifanyie kwanza mkate mdogo ukaniletee; kisha ujifanyie nafsi yako na mwanao. Kwa kuwa Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, Lile pipa la unga halitapunguka, wala ilc chupa ya mafuta haitaisha, hata siku ile Bwana atakapoleta mvua juu ya nchi. Basi akaenda, akafanya kama alivyosema Eliya; na yeye mwenyewe, na Eliya, na nyumba yake, wakala siku nyingi.
Lile pipa la unga halikupunguka, wala ile chupa ya mafuta haikuisha, sawasawa na neno la Bwana alilolinena kwa kinywa cha Eliya.
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 4 :1-4, 6-7 (K) 6
(K) Bwana, utuinulie nuru ya uso wako.
Ee Mungu wa haki yangu, uniitikie niitapo;
Umenifanyizia nafasi wakati wa shida;
Unifadhili na kuisikia sala yangu.
Enyi wanadamu,
hata lini utukufu wangu utafedheheka? (K)
Bali jueni ya kuwa Bwana amejiteulia mtauwa;
Bwana atasikia nimwitapo.
Mwe na hofu wala msitende dhambi,
Tafakarini vitandani mwenu na kutulia. (K)
Wengi husema, Nani atakayetuonyesha mcma?
Bwana, utuinulie nuru ya uso wako.
Umenitia furaha moyoni mwangu,
Kupita yao wanapozidishiwa nafaka na divai. (K)
SHANGILIO
Zab. 27:11
Aleluya, alcluya, Ee Bwana, unifundishe njia yako, na kuniongoza katika njia iliyonyoka. Aleluya.
INJILI
Mt. 5:13-16
Yesu aliwaambia wanafunzi wake: Ninyi ni chumvi ya dunia; lakini chumvi ikiwa imeharibika itatiwa nini hata ikolee? Haifai tena kabisa, ila kutupwa nje na kukanyagwa na watu. Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima. Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango; nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani. Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.
Copyright © 2026, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania. Readings reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com

No comments:
Post a Comment