“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Ijumaa, 30 Januari 2026,
Juma la 3 la mwaka
2 Sam 11: 1-10, 13-17;
Zab. 51: 3-7, 10-11;
Mk 4: 26-34.
KUSIMIKA UFALME WA MUNGU!
Leo tena Yesu anaongelea jambo jingine, mtu aliepanda mbegu ardhini nakuisubiri ichipue nakumea mpaka ichanue nakuwatayari kwa mavuno. Hajui ni jinsi gani inavyoota lakini anavuna wakati wa mavuno utimiapo.
Yesu pia anaongelea kuhusu punje ya Haradali ambayo ni ndogo sana lakini hukuwa na kuwa mmea mkubwa, hata kuwa na msitu wakuweza kukaa ndege juu yake na kuweka viota ndani yake.
Mfano huu unaelezea maadili au ukweli wa kiroho ambao Yesu alikuwa akiwafundisha wafuasi, kwamba yeye anafanya nini na wao inawapasa wafanye nini wakati utakapo timia. Neno hili ambalo ni ujumbe na nafsi ya Yesu lina nguvu, linatawala kwa nguvu sehemu nyingi na linapenya na kuwa kitulizo kinacho wajenga wengine na kuwalinda na kuwahifadhi wadogo katika dunia yetu.
Ufalme wa Mungu unafanya kazi namna hiyo hiyo kati yetu, bila hata kutambua kwa akili zetu, lakini je, tupo tayari kuvuna katika shamba hili la neema au tupo tayari kulala katika shamba la dhambi lililo jaa majani? Je tunatambua kuwa tunaweza kutenda jambo jema dogo sana likakua likaleta neema kwako na kwa wengine?
Sala :Bwana, naomba nioteshe matendo mema, ili yaweze kuwa mavuno ya Neema kwa watu wote. Amina.
No comments:
Post a Comment