SOMO 1
Bar 1:15-22
Kwa Bwana
Mungu wetu, haki; lakini kwetu sisi haya ya uso kama hivi leo, kwa watu wa Yuda
na kwa wenyeji wa Yerusalemu, na kw awafalme wetu, na kwa wakuu wetu, na kwa
makuhani wetu, na kwa manabii wetu, na kwa baba zetu, kwa sababu tumetenda
dhambi mbele ya Bwana. Tumemwasi, wala hatukuitii sauti ya Bwana Mungu wetu,
kwenda katika sheria zake alizoziweka mbele yetu. Tangu siku Bwana aliyowatoa
baba zetu katika nchi ya Misri hata leo tumemwasi Bwana Mungu wetu na kutenda
yasiyofaa kwa kutoisikiliza sauti yake. Kwa hiyo mapigo haya yameshikamana
nasi, na ile laana ambayo Bwana alimwamuru mtumishi wake Musa, katika siku
aliyowaleta baba zetu kutoka katika nchi ya Misri ili atupe nchi ijaayo maziwa
na asali, kama hivi leo. Lakini hatukuisikiliza sauti ya Bwana Mungu wetu, kwa
kuyafuata maneno yote ya manabii aliyotupelekea, bali tulikwenda kila mtu
katika mawazo ya moyo wake mbaya, kutumikia miungu ya kigeni na kufanya yaliyo
maovu machoni pa Bwana Mungu wetu.
Neno la Bwana...Tumshukuru
Mungu
WIMBO WA
KATIKATI
Zab.
79:1-6, 8-9
(K)
Utusaidie, Ee Mungu, kwa ajili ya utukufu wa jina lako.
Ee Mungu,
mataifa wameingia katika urithi wako,
Wamelinajisi
hekalu lako takatifu.
Wamefanya
Yerusalemu chungu chungu.
Wameziacha
maiti za watumishi wako
Ziwe
chakula cha ndege wa angani.
Na miili ya
watauwa wako Iwe chakula cha wanyama wa nchi. (K)
Wamemwaga
damu yao kama maji
Pande zote
za Yerusalemu,
Wala
hapakuwa na mzishi.
Tumekuwa
lawama kwa jirani zetu,
Mzaha na
dhihaka kwao wanaotuzunguka.
Ee Bwana,
hata lini? Utaona hasira milele?
Wivu wako
utawaka kama moto? (K)
Usikumbuke
juu yetu maovu ya baba zetu,
Rehema zako
zije kutulaki hima.
Kwa maana
tumedhilika sana. (K)
Ee Mungu wa
wokovu wetu, utusaidie,
Kwa ajili
ya utukufu wa jina lako.
Utuokoe,
utughofiri dhambi zetu,
Kwa ajili
ya jina lako. (K)
SHANGILIO
Yn 10:27
Aleluya,
aleluya,
Kondoo
wangu waisikia sauti yangu, nami nawajua, nao wanifuata.
Aleluya.
INJILI
Lk 10:13–16
Yesu
aliwaambia wafuasi wake: Ole wako, Korazini! Ole wako, Bethsaida! Kwa kuwa kama
miujiza hiyo iliyofanyika kwenu ingalifanyika katika Tiro na Sidoni,
wangalitubu tangu hapo, huku wakiketi katika nguo za kigunia na majivu. Lakini,
siku ya hukumu itakuwa rahisi Tiro na Sidoni kustahimili adhabu zake kuliko
ninyi. Nawe Kapernaumu, je! Utakuzwa hata mbinguni? Utashushwa hata kuzimu.
Awasikilizaye ninyi anisikiliza mimi, naye awakataaye ninyi anikataa mimi; naye
anikataaye mimi amkataa yeye aliyenituma.
Neno la Bwana...Sifa kwako, ee Kristo
🙏🏽
ReplyDelete