Everyday Saint / Maisha ya Watakatifu

--KUPONYWA KWA UPOFU--

 


“KWARESIMA YA UKARIMU”
Tafakari ya Kwaresima
Jumapili, Machi 19. 2023.
Dominika ya 4 ya Kwaresima

1Sam 16: 1, 6-7,10-13;
Zab 23: 1-6;
Ef 5: 8-14;
Yn 9: 1-41.


KUPONYWA KWA UPOFU


Kulikuwa na kijana mmoja alyezaliza kipofu katika kijiji kimoja. Kila siku jioni alikuwa akichukua taa ili kuvuka msitu mmoja wenye giza kuelekea nyumbani kwake. Mtu mmoja mpita njia alikutana na huyu kipofu akamuuliza swali “je, wewe si kipofu; sasa inakuwaje umebeba taa?’ Yule kipofu akajibu akasema hii taa ni kwa ajili yenu ili msije mkagongana na mimi.

Katika maisha, macho yenye afya hayawezi kuona yote. Tunaweza kuona vitu vingine tunapokuwa na wengine. Elimu ya kisayansi ambayo inaweza kutusaidia kuchunguza na kujaribu yale yote yanayo shikika, na kutufanya tuwe na hali ya kutaka kujua zaidi, kufurahia na kuamini yote yanayo onekana kwa macho, kugundulika kwa kutumia milango ya fahamu, na kuangalia na vyombo vya maabara na kusema ni kweli. Kuna upofu mwingine pia ambao umejikita katika mizani ya ulimwengu,: pesa, mafanikio, kazi, mapenzi, afya na ugonjwa, ujana na uzee n.k. lakini uwezo wa kuamini kuona vizuri unafunga ndani na macho ya kiroho yanayo tusaidia kuzama katika mafumbo ya Mungu, maana ya maisha na kifo, na kilele cha historia ya mwanandamu.

“Mwanga wa kweli unao mwangaza kila mtu umekuja ulimwenguni” (Yn 1:9). Yesu alikuja kufukuza giza letu, kuangaza usiku wetu, kukaa katika “watoto wa mwanga na watoto wa mchana” (1 Thes 5:5). Tunaitwa kuangalia katika upofu wetu wa roho. Tunaitwa kuushinda kwa kufungua macho yetu ya kiroho.

Katika somo la kwanza tunamwona Mfalme Sauli anashindwa kumtii Mungu. Anakiuka amri za Mungu, Sauli alimhifadhi Mfalme wa Ameleki na kujipatia vingi kwasababu ya vita. Ndipo Mungu akamkataa Sauli akamtuma Samueli kwenda katika mji wa Bethlehemu kumchagua Mfalme atakaye muonesha. Samueli anaenda katika nyumba ya Yese na baada ya kumuona mtoto wa kwanza wa Yese ambaye alikuwa na nguvu, mzuri, na mrefu. Samueli alidhani huyu ndiye aliyechaguliwa na Bwana, na hapo anasikia sauti kwamba “Mungu haangalii kama Mwanadamu anavyo angalia; mwanadamu hutazama sura ya nje bali Mungu huangalia unyofu wa moyo”. Samueli anaoneshwa Daudi na anamchagua, akiwa ni mtoto wa mwisho wa Yese ambaye alikuwa akichunga kondoo. Wanadamu wana mambo mengi katika akili, ambayo hayawa saidii kufikia hitimisho.

“Upofu” ni kushindwa kuona mkono wa Mungu ukifanya kazi kati yetu. Tunakazana kutafuta miujiza ya Neema za Mungu zinazo onekana kwetu na kwa wengine. Kwahiyo kitu cha kwanza kabisa ambacho tunapaswa kufanya ndicho ambacho tunapata katika Injili ni kutambua upofu wetu. Ni lazima tukazane na kukubali kwamba tumeshindwa kumuona Mungu akiwa kazini akitenda kazi. Kukazana huku kutatusaidia kutambua na kutamani uponyaji wa kiroho. Kitu kizuri ni kwamba Yesu alimponya huyu mtu na kwamba atatuponya sisi pia. Kurudisha hali ya kuona ni rahisi sana kwa Yesu. Kwahiyo sala ya kwanza kabisa ambayo tunapaswa kuisali kutokana na ujumbe huu wa Injili “Bwana naomba niweze kuona” unyenyekevu wa kukiri upofu wetu utatusaidia Mungu aje kutenda kazi kwetu. Na kama hatutakiri kwa unyenyekevu upofu wetu, hatutakuwa katika nafasi ya kuomba uponyaji.

Alifanyaza tope kwa mate yake na kumpaka huyu kijana katika macho, kitendo hiki kina onesha kuwa ni ajabu. Lakini inaonesha kwamba Yesu anaweza kutumia kitu ambacho hatudhani kwa ajili ya kazi yake ya Kimungu. Ni mara nyingi tuna angalia kazi za Mungu katika hali ya juu kabisa. Lakini ni mara nyingi yupo nasi katika yale ya kawaida. Pengine tunaweza kushawishika kufikiri kwamba Mungu anafanya matendo yake kwa njia ya upendo au sadaka. Pengine tunaweza kushawishika kudhani kwamba Mungu hawezi kutumia mambo yetu ya kawaida kutenda miujiza yake. Lakini hili si kweli. Ni hakika kabisa maisha ya kawaida na vitu vya kawaida kabisa katika maisha ndipo Mungu alipo. Kwa hakika, kazi inapokuwa ya kwaida ndipo tukazane zaidi kuona Mungu akitenda kazi. Na tutakapo “muona” yeye akiwa katika mambo ya kawaida ya maisha, tunakuwa tumeponywa na upofu wetu wa roho.
               
Sala: Bwana, ninaomba nione. Nisaidie mimi niponywe na upofu wangu. Nisaidie mimi niweze kukuona katika kila kazi ya maisha yangu. Ninaomba unisaidie niweze kukuona katika matukio madogo ya kila siku katika maisha. Na ninapo kuona wewe ukiwa ndani, jaza Moyo wangu kwa shukrani kwa kuona huku. Yesu, nakuamini Amina


Copyright ©2013-2023 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.

No comments:

Post a Comment