“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari
ya kila siku
Jumanne,
Februari 15, 2022,
Juma
la 6 la Mwaka wa Kanisa
Yak
1:12-18
Zab
94:12-15.18-19;
Mk
8: 14-21.
CHACHU
ULIMWENGUNI!
Karibuni ndugu zangu kwa adhimisho la Misa Takatifu. Leo neno la Bwana
katika asubuhi ya leo tutaanza kwa kuliangalia somo la kwanza ambapo tunakutana
na fundisho juu ya faida za majaribu. Yakobo anakubali kwamba majaribu yapo,
lakini atakayeweza kukabiliana nayo hadi mwisho huyo hukubalika kwa Mungu na
hujipatia tuzo kuu. Mtu wa namna hii ni yule awezaye kuona faida iliyopo katika
vishawishi, yaani kuiimarisha Imani ya mwanadamu. Na hili kweli ni jambo ambalo
maishani tunakumbana nalo. Ukikutana na mtu ambaye majaribu kama magonjwa
yamekuja kwake na kwa njia ya yale majaribu ameikweza ile imani yake-kwa kweli
huyu huwa ni wa pekee. Huyu huwa siku zote ni imara katika imani, hayumbishwi
na vitu vidogo vidogo ndani ya imani yake. Huyu kweli huwa na Imani. Ni kama
shahidi aliyeepukika kifo. Lakini ukikutana na yule ambaye hajawahi kukutana na
majaribu yoyote, kwa kweli imani yake mara nyingi huwa ni dhaifu na huwezi
kujua kwamba kweli huyu mtu ana imani au anafuata mkumbo. Halafu kuna wale
wengine ambao majaribu yamekuja na kuwafanya wapoteze Imani, wanabadilika
kabisa. Walipokuwa bila majaribu, walikuwa wanakuja kanisani kila siku lakini
baada ya majaribu, hata kanisani hawafiki. Mtu wa namna hii huwezi kusema
kwamba alikuwa na imani kubwa kwa Mungu. Mungu ameruhusu majaribu kutaka imani
yake na mtazamo wake wa imani ubadilike, uimarike lakini kwa sababu yeye
alikuwa na vionjo vyake na mategemeo yake kama Yakobo anavyotueleza katika somo
la kwanza, basi akaishia kupoteza.
Ndugu zangu, Imani yetu lazima iimarishwe na majaribu-na majaribu
yanapokuja, mtakatifu yakobo anasema lazima tuyakubali kwani aliyekwisha pokea
majaribu huyo anayo imani bora kuliko yule ambaye hajawahi kuona jaribu lolote.
Hivyo yabidi kufurahia majaribu.
Na hili suala la majaribu tunakutana nalo tena katika injili. Tutasikia
katika injili wanafunzi wa Yesu wakiogopa kwa sababu hawakuchukua mikate.
Wanajiuliza kwamba je, tutakula nini? Mbona itakuwa njaa tu huku? Wanajilaumu.
Lakini Yesu anasikitika. Anaona kwamba kumbe hawa watu wake hawana imani. Yaani
wamekwisha niona nikitenda miujiza mingi na kumbe ile miujiza walikuwa hata
hawaitilii maanani? Kumbe walikuwa hawaoni kana kwamba nalikuwa natenda
miujiza? Hivyo, Yesu anasikitika kwa sababu wanachukulia vitu kimzaha mzaha
mno. Anaona kwamba matendo yake yote anayowafanyia hayawajengi kiimani. Hivyo,
Watu KAMA HAWA WANGEHITAJI MAJARIBU YA MMOJA MMOJA ILI WAMTAMBUE YESU KUWA NI
NANI. ILE MIUJIZA YA PAMOJA INAWAFANYA WENGINE WASHINDWE KUMSHUHUDIA AU
KUMTAMBUA YESU KWA SABABU LABDA ANAPOKUWA ANAITENDA WENGINE UNAKUTA WAKO BUSY
NA MAMBO YAO NA NDIO MAANA HAWAWEZI KUJIFUNZA TOKA KWA HIYO MIUJIZA. HIVYO,
WALIHITAJI JABIBU MOJA MOJA LIWAFUNZE.
Hivyo ndugu zangu leo tunaalikwa kuangalia majaribu yote ambayo tumewahi
kukutana nayo maishani. Yaangalie, ona kama yamewahi kukuimaraisha. Kama
yameshindwa kukuimaraisha lazima ubadilike. Hapa ni kukosa imani kama hawa
mitume wa leo. Usikubali ugonjwa, au jaribu lolote likufanye uwe sababu ya wewe
kushindwa kiimani. Tusimtukane Mungu, Yakobo anatuambia kwamba Imani yetu
ikiimarishwa kwa njia ya majaribu, basi tutastahili tuzo kubwa. Maneno haya
yatutie moyo kuvumilia majaribu yetu.
Copyright
©2013-2022 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment