MASOMO YA MISA, JANUARI
11, 2022
JUMANNE, JUMA LA 1 LA
MWAKA
SOMO 1
1Sam. 1:9-20
Walipokwisha kula na
kunywa huko Shilo Hana akainuka. Naye Eli, kuhani, alikuwa akiketi kitini pake
penye mwino wa hekalu la Bwana. Naye huyo mwanamke alikuwa na uchungu rohoni
mwake, akamwomba Bwana, akalia sana. Akaweka nadhiri, akasema, Ee Bwana wa
majeshi, ikiwa wewe utaliangalia teso la mjakazi wako, na kunikumbuka, wala
usinisahau mimi mjakazi wako, na kunipa mimi mjakazi wako mtoto mume, ndipo
mimi nitakapompa Bwana huyo mtoto siku zote za maisha yake, wala wembe
hautamfikilia kichwani kamwe.
Ikawa, hapo alipodumu
kuomba mbele za Bwana, Eli akamwangalia kinywa chake. Basi Hana alikuwa akinena
moyoni mwake; midomo yake tu ilionekana kama anena, sauti yake isisikiwe; kwa
hiyo huyo Eli alimdhania kuwa amelewa. Ndipo Eli akamwambia, Je! Utakuwa mlevi
hata lini? Achilia mbali divai yako. Hana akajibu, Hasha! Bwana wangu, mimi ni
mwanamke mwenye roho ya huzuni; mimi sikunywa divai wala kileo, ila nimeimimina
roho yangu mbele za Bwana. Usimdhanie mjakazi wako kuwa ni mwanamke asiyefaa
kitu; kwa kuwa katika wingi wa kuugua kwangu na kusikitika kwangu ndivyo
nilivyonena hata sasa. Ndipo Eli akajibu, akasema, Enenda kwa amani; na Mungu
wa Israeli akujalie haja yako uliyomwomba. Naye akasema, Mjakazi wako na aone
kibali machoni pako. Basi huyo mwanamke akaenda zake, naye akala chakula, wala
uso wake haukukunjamana tena.
Wakaondoka asubuhi na
mapema, wakasali mbele za Bwana, kisha wakarejea na kufika nyumbani kwao huko
Rama; Elkana akamjua mkewe Hana; naye Bwana akamkumbuka. Ikawa, wakati
ulipowadia, Hana akachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; akamwita jina lake
Samweli, akisema, kwa kuwa nimemwomba kwa Bwana.
Neno la Bwana…
Tumshukuru Mungu.
WIMBO WA KATIKATI
1Sam. 2:1,4-5,6-7,8
(K)1
(K) Moyo wangu
wamshangilia Bwana.
Moyo wangu wamshangilia
Bwana,
Pembe yangu imetukuka
katika Bwana,
Kinywa change
kimepanuka juu ya adui zangu,
Kwa kuwa naufurahia
wokovu wako. (K)
Pinde zao mashujaa
zimevunjika,
Na hao waliojikwaa wamefungiwa
nguvu.
Walioshiba
wamejikodisha ili kupata chakula,
Na hao waliokuwa na
njaa wamepata raha.
Naam, huyo aliyekuwa
tasa amezaa watoto saba,
Na yeye aliye na wana
wengi amedhoofika. (K)
Bwana huua, naye
hufanya kuwa hai;
Hushusha hata kuzimu
tena huleta juu.
Bwana hufukarisha mtu
naye hutajirisha;
Hushusha chini tena
huinua juu. (K)
Humwinua mnyonge kutoka
mavumbini,
Humpandisha mhitaji
kutoka jaani,
Ili awaketishe pamoja
na wakuu,
Wakakirithi kiti cha
enzi cha utukufu,
Kwa maana nguzo za
dunia zina Bwana. (K)
SHANGILIO
1Tim. 2:13
Aleluya, aleluya,
Lipokeeni Neno la
Mungu, siyo kama neno la wanadamu, bali kama Neno la Mungu.
Aleluya.
INJILI
Mk. 1:21-28
Yesu na wanafunzi wake
walishika njia mpka Kapernaumu, na mara siku ya sabato akaingia katika sinagogi,
akafundisha. Wakashangaa mno kwa mafundisho yake; kwa maana alikuwa akifundisha
kama mtu mwenye amri, wala si kama waandishi.
Na mara palikuwapo
ndani ya sinagogi lao mtu mwenye pepo mchafu; akapaza sauti, akisema Tuna nini
nawe, Yesu wa Nazareti? Je! Umekuja kutuangamiza? Nakutambua u nani, Mtakatifu
wa Mungu. Yesu akamkemea, akisema, Fumba kinywa, umtoke. Yule pepo mchafu
akamtia kifafa, akalia kwa sauti kuu, akamtoka. Wakashangaa wote, hata
wakaulizana, wakisema, Nini hii? Ni elimu mpya! Maana kwa uweza awaamuru hata
pepo wachafu, nao wamtii! Habari zake zikaenea mara kotekote katika nchi zote
kandokando ya Galilaya.
Neno la Bwana… Sifa
kwako Ee Kristo
-------------------------
Copyright
© 2022, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment