“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Januari
11, 2022.
------------------------------------------------
JUMANNE,
JUMA LA 1 LA MWAKA
Somo
la 1: 1 Sam 1:9-20 sala ya Hanna inajibiwa na Bwana. Anabarikiwa kwa kuwa na
mtoto wa kiume ambaye jina lake ni Samueli, “kwani alimuomba Mungu”.
Wimbo
wa Katikati Zab: 1 Sam 2:1,4-8 Moyo wangu wamtukuza Bwana, nafurahia mkono wake
wa wokovu.
Injili:
Mk 1:21-28 Yesu anamponya mtu mmoja aliyekuwa na pepo Wabaya.
------------------------------------------------
KUISIKILIZA
SAUTI YA MUNNGU !
Leo
tunamwona Yesu anaanza utume wake kufundisha watu katika sinagogi. Alifundisha
kwa mamlaka makubwa zaidi kuliko walimu wao wa kawaida. Alikutana na mtu mwenye
pepo mchafu, ambao walianza kumpigia kelele Yesu: "Tuna nini nawe, Je!
umekuja kutuangamiza? Nakutambua u nani, Mtakatifu wa Mungu."
Yesu
anaongea kwa mamlaka makubwa si kwamba alitaka, bali ndivyo alivyo. Yeye ni
Mungu na wakati anaongea anaongea kwa mamlaka ya Kimungu. Anaongea katika hali
kwamba maneno yake yana gusa mioyo ya watu na kutaka mabadiliko. Hata pepo
wabaya wanatambua mamlaka ya Yesu.
Hili
linapaswa kutualika kila mmoja wetu kutafakari juu ya mamlaka ya Yesu katika
maisha yetu. Yesu anatamani daima kuongea nawe katika moyo wako na kubadili
maisha yako awe nawe akiongea katika mamlaka. Tunaomba maneno yake yazame ndani
mwetu yabadili maisha yetu.
Hali
kadhalika nasi katika maisha yetu ya kiroho, sisi wenyewe nguvu tuliyopewa na
Yesu. Sisi ni watoto wa Mungu. Yule mwovu hutujaribu, anajaribu kutuvuruga sisi
na vurugu, fujo na uongo. Je! Tuna nguvu ya kutosha kusimama dhidi yake?
Sala:
Bwana, nafungua Moyo wangu juu ya sauti yako ya mamlaka yako. Nisaidie mimi
nikuruhusu uongee kwa mamlaka na ukweli. Ukiwa unafanya hayo, nisaidie mimi
kubadili maisha yangu na kushinda uovu wote kwa njia ya neema yako. Yesu,
nakuamini wewe. Amina
Copyright
©2013-20202 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment